Kwa mujibu wa mashuhuda, ajali hiyo ilitokea majira ya saa 12 asubuhi ya leo februari 22, 2023 ilihusisha gari dogo aina ya Rav 4 lenye namba za usajili T978DHZ inayodaiwa kumilikiwa na shirika la ndege la RwandAir
Aidha, uongozi wa DART umewataka madereva wote wakiwemo wa wakala huo na wale wa magari binafsi kuzingatia sheria za usalama barabarani, ili kuepuka ajali, vifo na hasara.
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
WATU kadhaa wameripotiwa kujeruhiwa asubuhi ya leo baada ya basi la abiria la ‘mwendokasi’ lenye namba za usajili 122 DGW lililokuwa likiendeshwa na Shabani Ngaugia kugongana na gari dogo aina ya Toyota Rav4 eneo la Kisutu Jijini Dar es salaam, Mashuhuda wameeleza.
Kwa mujibu wa mashuhuda, ajali hiyo ilitokea majira ya saa 12 asubuhi ya leo Februari 22, 2023 iliyohusisha gari dogo aina ya Toyota Rav 4 lenye namba za usajili T978DHZ inayodaiwa kumilikiwa na shirika la ndege la Rwanda (RwandAir).
Mashuhuda hao walieleza kuwa dereva wa mwendokasi alikuwa akitokea Kivukoni kwenda Kimara ambapo alipofika kwenye mataa ya mtaa wa Kisutu gari ndogo hiyo iliyokuwa inapita pasipo kuangalia dereva wa mwendokasi alimuona na wakati akimkwepa ndipo alipoenda kugonga maduka pamoja na mtembea kwa miguu.
Mashuhuda wamesema kuwa dereva wa gari hilo dogo hakuzingatia sheria za barabarani kitendo kilichosababisha kugongwa na basi hilo lililokuwa likitokea maeneo ya Kivukoni
Wameeleza kuwa, dereva wa basi hilo alijitahidi kulikwepa gari dogo lakini jitihada hizo hazikuzaa matunda kwani pamoja na kuligonga gari hilo aliishia kugonga ukuta wa jengo lililokuwepo upande wa kulia sambamba na mtembea kwa miguu.
Mashuhuda wameeleza kuwa ndani ya basi la mwendokasi kulikuwa na abiria ambao wengi ni wanafunzi ambao walijeruhiwa na kukimbizwa hospitali ta Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu.
Aidha mashuhuda wameeleza kuwa dereva wa basi la mwendokasi alipata majeraha makubwa miguuni.
Baada ya ajali hiyo kutokea waliokuwa ndani ya gari hiyo ndogo waliumia na kupelekwa hospitali dereva wa gari ndogo alivyofika hospitali alikimbia akabaki majeruhi mmoja ambaye ni mwanamke.
Wakati huo huo , Wakala wa Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam (DART) umeomba radhi kufuatia ajali ya basi lake na gari dogo aina ya Toyota RAV4
Pia uongozi wa DART umewataka madereva wote wakiwemo wa wakala huo na wale wa magari binafsi kuzingatia sheria za usalama barabarani, ili kuepuka ajali, vifo na hasara.
