NAIROBI, KENYA
Mchekeshaji Eric Omondi na wenzake 17 wamepandishwa kizimbani kwenye mahakama jijini Nairobi wakidaiwa kujihusisha na mkusanyiko haramu.
Inadaiwa Omondi na wenzake 17 walikamatwa jana walipokuwa kwenye maandamano barabara ya bunge wakiwa nau jumbe wa kutaka serikali ipunguze ukali wa maisha kufuatia mfumuko wa bei za bidhaa nchini humo.
Watuhumiwa wote 18 wamekanusha shitaka na wameachiwa kwa dhamana ya Tsh. 400,000.
Wakili wa akina Omond, Danstan Omari amesema hati ya mashitaka inasomeka kuwa wateja wake wanashtakiwa kwa kufanya mkusanyiko haramu karibu na bunge.
Walikuwa wanakwenda Bungeni kupata ufumbuzi wa tatizo la kupanda kwa gharama za maisha. Naitaka mahakama ifahamu kuwa wapo Wakenya Milioni 6 wanaoshinda njaa,” alisema Omari
Omondi na wenzake 17 tote ni wasanii wa runinga

PICHA KWA HISANI YA THE STAR