Wananchi hao wanasema mara nyingi wawanapokamatwa hufikishwa katika Kituo cha Polisi Ifakara lakini lugha wanazopewa sio za kiuungwana huku wengine wakiwatuhumu kushirikiana na Watu wenye fedha na kuwapokonya haki Wananchi wanyonge.
Baada ya malalamiko hayo Masauni akatoa msimamo wa Serikali ambapo ameswasimamisha kazi na kuwahamisha Maofisa hao ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazotolewa za Wananchi kwa Jeshi la Polisi.
Masauni amenukuliwa akisema “Hivi karibuni tumewahamisha Askari Polisi wengi katika Mkoa huu akiwemo aliyekuwa RPC, Fortunatus Musilimu na sasa tumemleta Kamanda mwingine Alex Mkama hivyo sitarajii turudi tulikotoka niseme tu kwamba Askari mmoja akichafua Jeshi tutamshughulikia kama Mhalifu ili asiharibu taswira ya Jeshi letu”