SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF), limeufungia Uwanja wa Benjamini William Mkapa uliopo jijini Dar es Salaam kutotumika kwenye mechi za shirikisho hilo wakidai umeharibika nyasi za kuchezea (pitch).
Kwa mujibu wa Meneja wa Uwanja huo, Salum Mtumbuka amesema baada ya mechi mbili za CAF zilizochezwa Jumamosi na Jumapili iliyopita walikutana na maofisa wa CAF ambao waliwapa maelekezo namna ya kufanya marekebisho hasa eneo la kuchezea.
Tulikubaliana kwa pamoja na CAF kwamba wakati marekebisho yanaendelea ambayo yatachukua muda wa mwezi mmoja, mechi zitakazochezwa kwenye uwanja wa Mkapa ni zile za kimataifa za CAF na timu ya Taifa, mechi zingine za ligi kuu wanaotumia uwanja huu watatafuta viwanja vingine,” alisema Mtumbuka
Uwanja huko wa Mkapa unatumika na vilabu via Simba na Yanga kama uwanja wao wa nyumbani.