NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
WAZIRI wa Fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayeiwakilisha Tanzania kwenye Benki hiyo, Jonathan Nzayikorera.
Dk Nchemba amekutana na Mkurugenzi huyo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, akiwa safarini kuelekea Bujumbura nchini Burundi, kuhudhuria Mkutano wa 43 wa Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, utakaofanyika februari 23, 2023.
Nzayikorera amewasili nchini leo februari 21 kwa ziara ya kikazi ya siku nne, ambapo pamoja na mambo mengine atakagua maendeleo ya miradi inayofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika.