Wakati vita kati ya Rusia na Ukraine ikiendelea, Rais wa Marekani, Joe Biden amewasili nchini Ukraine kimya kimya na kutembelea maeneo mbalimbali.
Safari hiyo ya kwanza ya Biden nchini Ukraine kama Rais inawadia siku chache kabla ya maadhimisho ya mwaka mmoja wa vita kati ya Ukraine na Urusi.
Akizungumza mara baada ya kuwasili, Biden alisema Rais wa Urusi, Vladimir Putin alikuwa amekosea kufikiria kuwa nchi yake inaweza kuishinda Ukraine na washirika wake wa Magharibi.
Biden ameonekana akiwa na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky na wawili hao walitembelea eneo la kumbukumbu ya wanajeshi waliofariki katika kipindi cha miaka tisa tangu Urusi ilipotwaa eneo la Crimea na vikosi vyake vilivyomuunga mkono kutwaa maeneo ya mashariki la Donbas.
Wadadisi wa mambo ya kisiasa wanaeleza kuwa ziara hiyo ya Biden inathibitisha kuwa Marekani inaiunga mkono Ukraine kwenye vita dhidi ya Urusi.
Rais huyo wa Marekani alikuwa amesafiri kwa treni kwa saa 10 kutoka Poland hadi kufika Kyiv kwa siri, kisha akarudi Poland.
Baada ya ziara hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken alitangaza kupa nchi yeke imeipatia Ukraine msaada wa Dola za Marekani Milioni 450 (Tsh. Trilion 1.1), ikiwa ni pamoja na silaha za howiters, mfumo wa roketi wa Himars, makombora ya Javelin na rada za uchunguzi wa anga.
Marekani pia itaipatia Ukraine msaada wa ziada wa Dola za Marekani Milioni 10 (Tsh. Bilioni 230) kwa ajili ya kupata nishati na Tsh. Bilioni 230 nyingine kwa jailli ya kukarabati miundombinu ya nishati.