Home
Burudani
Kimataifa
Kitaifa
Magazeti
Mchanganyiko
Michezo
Siasa
Uchumi
Burudani
Kimataifa
Kitaifa
Magazeti
Michezo
Siasa
Uchumi
Home
Burudani
Kimataifa
Kitaifa
Magazeti
Mchanganyiko
Michezo
Siasa
Uchumi
Have an existing account?
Sign In
Follow US
Afya
Latest Afya News
JKCI Dar Group na Cardiostart International wafanya kambi maalumu Na Mwandishi Maalumu ,Dar es Salaam Kwa mara ya kwanza Hospitali ya JKCI Dar Group kwa kushirikiana na wataalamu wa afya kutoka Shirika la Cardiostart International la nchini Marekani wamefanya kambi maalumu ya upimaji wa vipimo vya moyo kwa wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam.Upimaji huo umefanyika kwa siku mbili ambapo wananchi waliojitokeza wamepata fursa ya kupima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) pamoja na kipimo cha kuangalia mfumo wa umeme wa moyo (Electrocardiography – ECG) bila malipo.Akizungumza na mwandishi wa habari hii daktari wa Hospitali ya JKCI Dar Group Marsia Tillya alisema uhitaji wa wananchi kupata huduma ya vipimo vya moyo ni mkubwa kutokana na idadi kubwa ya wananchi waliojitokeza kupima kufanya vipimo hivyo.Dkt. Marsia alisema watu waliojitokeza kufanya vipimo hivyo wapo ambao walishawahi kupima na kukutwa na magonjwa ya moyo lakini kutokana hali zao za uchumi hawakupata nafasi ya kupima tena hadi nafasi hiyo ilipojitokeza.“Watu tuliowaona wapo ambao walishapima na kukutwa na shida za moyo lakini pia wapo watu ambao hawakuwahi kupima moyo lakini kupitia kambi hii wamepata fursa ya kupima na kufahamu hali zao”, alisema Dkt. MarsiaKwa upande wake mtaalamu wa afya kutoka Shirika la Cardiostart International la nchini Marekani Sarah King alisema wataalamu wa afya wa Cardiostart mbali na kutoa huduma za upasuaji wa moyo pia walijipanga kufanya vipimo vya moyo kwa wananchi bila malipo kuwapa nafasi ya kuchunguza mioyo yao.“Tumepanga kufanya vipimo vya moyo kwa watu wote watakaojitokeza hivyo wasisite kufika katika Hospitali ya Dar Group kwani tupo kwaajili yao”, alisema Sarah.Sarah alisema sambamba na kuwafanyia wananchi vipimo vya moyo pia wanapata muda wa kuzungumza na wananchi wanaofika katika kambi hiyo kufahamu masuala muhimu ya afya zao na kuwajengea tabia za kupima afya zao mara kwa mara kabla ya kuumwa.Naye mwananchi aliyepatiwa huduma katika kambi hiyo Susan Paul alisema amejitokeza kupima moyo wake kutokana na hapo awali alipata maumivu makali ya moyo na kufika katika moja ya hospitali ambapo alipatiwa huduma na kushauriwa kupima moyo wake.Susan alisema baada ya kupata tangazo la upimaji wa vipimo vya moyo katika Hospitali ya Dar Group aliona hiyo ndio fursa kwake kufika na kupima moyo wake ili aweze kujua afya yake.“Nashukuru sana kwa hii nafasi niliyoipata kuchunguza moyo wangu mapema kwani kunanipa nafasi ya kujua kama lile tatizo nililokuwa nalo awali linasababishwa na magonjwa ya moyo na kama sio nitajilinda ili nisije kupata ugonjwa huu wa moyo”alisema Susan.
Editor
March 15, 2024
JKCI YAOMBWA KUTOA ELIMU YA LISHE NA MWANDISHI MAALUMU,DAR ES SALAAM WANANCHI wa Mkoa wa Dar es Salaam wameiomba Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kuendelea kutoa elimu ya lishe bora ambayo itawasaidia kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo magonjwa ya moyo.Ombi hilo limetolewa leo Machi 4,2024 jijini Dar es Salaam wakati wa kambi maalumu ya upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo inayofanywa na wafanyakazi wa Taasisi hiyo katika Hospitali ya JKCI Dar Group.Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi waliopata huduma katika kambi hiyo walisema licha ya kupata huduma za matibabu pia wamefurahia kupata elimu ya lishe ambayo imewasaidia kufahamu namna bora ya kuchagua makundi ya vyakula. Mzee Abdalah Yasini mkazi wa Temeke alisema inawezekana kupatwa kwake kwa tatizo la mishipa ya damu kuziba kulisababishwa na kutokupata elimu ya lishe bora kwani angejua toka zamani namna ya kula chakula chenye mchanganyiko wa makundi yote ya vyakula kwa kiasi angeweza kuepuka tatizo la mishipa yake ya damu kuziba.“Ninawaomba wataalamu wa lishe watafute namna ya kufikisha elimu ya lishe bora kwa jamii hata ikiwezekana katika vyombo vya habari kuwe na kipindi cha lishe kitatusaidia sana”, alisema Mzee AbdalahMzee Abdalah alisema kama jamii itazingatia lishe bora kwa kutumia makundi yote ya vyakula kwa kiasi kutasaidia kupunguza magonjwa yasiyoambukiza na kuwa na jamii yenye afya bora. Mama Yusta Joseph mkazi wa Kimbiji Dar es Salaam alisema elimu ya lishe aliyoipata inaenda kumbadilisha kwa kiasi kikubwa kwani kuna vitu amekuwa akivifanya ili kupunguza uzito kumbe alikuwa akifanya kimakosa.“Elimu niliyoipata leo itaenda kunisaidia kwani nilikuwa najitahidi kupambana kupunguza uzito kwa kutumia njia ambayo si sahihi, nilikuwa sili milo ya asubuhi na mchana nakula usiku tu lakini nilivyofika hapa mtaalamu amenipa maelekezo kuwa ninapokula jioni na kwenda kulala sehemu kubwa ya chakula hutunzwa kama mafuta”, alisema YustaYusta alisema mtaalamu wa lishe amemshauri kupunguza mlo wa jioni na namna ya kupata chakula bora kuanzi mlo wa asubuhi hadi jioni huku akimpa mbinu za kupunguza uzito wake bila ya kuleta athari nyingine za kiafya.“Kwakweli elimu niliyoipata leo haitakuwa ya msaada kwangu tu bali ninaenda kuisaidia familia yangu kwasababu mimi ndio mama yao na mimi ndio mpishi hivyo ninaenda kuwasaidi pia katika kuboresha afya zao”, alisema YustaMkuu wa Kitengo cha Lishe Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Maria Samlongo alisema wamekuwa wakitoa elimu ya lishe bora kwa wagonjwa wanaotibiwa katika taasisi hiyo pamoja na wananchi wanaohudumiwa katika kambi ambazo wamekuwa wakizifanya.Maria alisema wataendelea kushirikiana na vyombo vya habari ili kuhakikisha elimu ya lishe bora inawafikia wananchi wengi zaidi.“Bado elimu ya lishe haijaweza kuwafikia watu wote kutokana na uchache wa wataalamu wa lishe, kama JKCI tumetengeneza vipeperushi mbalimbali vinavyotoa elimu ya umuhimu wa lishe bora katika kupambana na magonjwa yasiyoambukiza”, alisema Maria Katika kambi hiyo jumla ya watu 364 walipatiwa huduma za upimaji wa magonjwa ya moyo ambapo kati yao watoto walikuwa 41 na watu wazima 323.Watoto 11 walikutwa na matundu kwenye moyo, shida za valvu na mishipa ya damu huku watu wazima 161 sawa na asilimia 50 walikutwa na matatizo ya shinikizo la damu pamoja na magonjwa mengine ya moyo ikiwemo mishipa ya damu na matatizo ya valvu za moyo.
Editor
March 4, 2024
Afya
TAARIFA YA NHIF KUHUSU UPATIKANAJI HUDUMA ZA MATIBABU BAADA YA KUANZA UTEKELEZAJI WA KITITA CHA MAFAO MWAKA 2023
Editor
March 1, 2024
1
2
…
4
5
6
Stay Connected
Facebook
Like
Twitter
Follow
Youtube
Subscribe
Telegram
Follow
- Advertisement -
Latest News
SERIKALI YAKARIBISHA WAWEKEZAJI SEKTA YA MADINI
Kitaifa
DK.HASHIL AIAGIZA MENEJIMENTI WMA KUTEKELEZA MAONO YA RAIS SAMIA
Kitaifa
BoT:AKIBA FEDHA ZA KIGENI IMEONGEZEKA
Uchumi
WAKALA WA VIPIMO WAZINDUA JARIDA LAO LA MTANDAONI
Kitaifa
Dismiss ad
This will close in
20
seconds
Welcome Back!
Sign in to your account
Username or Email Address
Password
Remember Me