Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.. Emmanuel John Nchimbi akisalimiana na kuzungumza jambo na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe, Dk Benson Kalikawe Lwakalinda Bagonza, baada ya ibada ya kuwekwa wakfu (kukaribishwa kazini) Askofu Dk Alex Gehaz Malasusa kuwa Mkuu Mpya wa KKKT, ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan alikuwa mgeni maalumu , iliyofanyika leo Jumapili, Januari 21, 2023, katika Kanisa la Azania Front, jijini Dar Es Salaam.