NA MWANDISHI MAALUMU, DAR ES SALAAM
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, Leo Juni 2023, amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan katika Swala ya Eid El Adh’haa ambayo imefanyika kitaifa Jijini Dar es Salaam katika Msikiti Mkuu wa Mfalme Mohamed wa Sita, uliopo Kinondoni.