NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
KUTOKANA na utaratibu wa mara kwa mara kwa kampuni ya michezo ya kubashiri Tanzania Meridianbet kuifikia jamii kwa kutoa kidogo wanachokipata ili kuchagiza shughuli za kimaendeleo juzi imetoa msaada wa vifaatiba na vifaa vya usafi kwenye Zahanati ya Kawe jijini Dar es salaam.
Akizungunmza na waandishi wa habari kwa niaba ya hospitali hiyo, Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Daktari Isack Mbalwa amesema
“Zoezi la meridianbet kufikia na kutoa kidogo wanachokipata kwenye faida yao kurejesha kwa jamii ni zoezi la kuigwa na makampuni mengine na hasa kwenye sekta ya afya, Ukizingatia bado kwenye sekta ya afya uhitaji wake ni wa kila siku, Hivyo tuna ishukuru meridianbet na tunaomba wasituchoke”
Naye Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Meridianbet Tanzania, Matina Nkurlu alisema “ Kama ilivyo kawaida ya Meridianbet Tanzania kuikumbuka jamii yake inayomzunguka na kutoa msaada katika maeneo mbalimbali kwenye jamii kama Polisi, Vijana wa boda boda, mama lishe na katika sekta hii ya afya leo hii tumewafikia ndugu zetu wa Zahanati ya Kawe, Leo imekua bahati sana kwakuwa ni sikukuu na kwenye siku na za namna hii ni lazima kuwe na utaratibu wa kupeana na kwa upande wetu tumeona tutoe kidogo tulicho nacho kwa Zahanati hii. ” alisema na kuongeza
“Napenda kuwahakikishia kwamba huu ni mwanzo tu wa zoezi hili sio mwisho tutarudi tena na tutaendelea kuwa karibu nanyi katika kujenga mahusiano yaliyo bora zaidi”
Aidha Nkurlu alibainisha kuwa ni ukweli usiopingika kwa Meridianbet Tanzania kuwa miongoni mwa kampuni kubwa nchini kwa kutoa mchango mkubwa katika sekta mbalimbali kusaidia jamii