NA DENIS CHAMBI, TANGA.
WIZARA ya kilimo imeipongeza Bodi ya Mkonge nchini(TSB) kwa namna inavyoendelea kutekeleza kwa vitendo na kusimamia mikakati iliyowekwa kwajili ya kuongeza uzalishaji wa zao hilo ambapo sasa uzalishaji umefikia tani 67 , 000 kutoka tani 48 mwaka 2018 huku mikoa inayolima zao hilo ikiongezeka .
Akizungumza katika ziara yake ya kutembelea mashamba ya mkonge mkoani Tanga katibu mkuu wizara ya kilimo Gerad Mweli amesema kuwa makubaliani waliyojiwekea na bodi ya mkonge ni kuongeza tija kwenye uzalishaji katika kila hekari inayolimwa , kuimarisha huduma za ugani kwa wakulima wa zao hilo ambapo lengo la serikali ifikapo mwaka 2025 ni kuhakikisha uzalishaji unafikia tani120, 000 moja na ishirini.
Amesema kuwa mwaka huu serikali imetoa kiasi cha shilingi billion 1.5 kwaajili ya kuiwezesha bodi ya mkonge nchini kuanzisha maeneo ya uchakataji wa zao hilo katika maeneo ya wilaya ya Handeni ambayo yameonekana uzalishaji wake ukiongezeka hii ni mara baada ya kuona kuwa baadhi ya wakulima wamekuwa wakivuna zao hilo mara moja kwa mwaka badala ya mara mbili kama inavyotakiwa
“Suala la uzalishaji wa Mkonge ni pana ambalo linaanzia shambani mpaka kwenye kiwanda , tumewekeana mikakati na tumekubaliana na bodi ya mkonge kuongeza tija kwenye uzalishaji, tunataka tuhakikishe tunaimarisha huduma za ugani kwa wakulima wetu na mikoa ambayo inalima katani imeongezeka uzalishaji wa hekta umeanza kuimarika kwa hekari na malengo ya serikali ni kufika tani 5 kwa mwaka 2025 “
“Tumefanya tathmini moja ya changamoto inayowakabili wakulima wetu ni uvunaji na usindikaji na mwaka huu serikali tumetoa shilingi billion 1.5 ambayo itawasaidia kwaajili ya usindikaji katika maeneo ya Handeni ambayo uzalishaji umeongezeka kwa kiasi kikubwa sana ili kuhakikisha nao wanakuwa na kiwanda kwaajili ya usindikaji” amesema Mweli.
Aidha ameongeza kuwa mpango uliopo kwa sasa ni kuongeza vifungashio ikiwemo kamba zinazotokana na zao la mkonge hii ikilenga kuondoa vifungashio vya plastiki hapa nchini ambapo lengo la serikali ni kuondoa na kuzuia vifungashio vinavyotana na plastiki vinavyotumika hapa nchini.
“Tumeanza na sisi wenyewe kuhakikisha kwamba tunaongeza uzalishaji wa vifungashio na kamba kabla hatujaanza kuzuia na kuhakikisha kwamba soko halitaathirika lakini tunaendelea kuwasiliana na taasisi nyingine simamizi ikiwemo NEMC ili kuhakikisha kwamba tunatekeleza jambo jili kwa ufanisi” aliongeza Mweli.
Kwa upande wake mkurugenzi wa bodi ya mkonge nchinj Saddi Kambona alisema kwa kupitia mradi wa BBT wa kuwainua vijana kiuchumi tayati wameshanzisha klabu za vijana waliopo mashuleni kuwafundisha namna bora watakayoitumia kupitia mabaki ya mkonge kujipatia kipato ikiwemo ufungaji wa Mende na kilimo cha uyoga.
“Bodi ya Mkonge kuna mikakati mingi sana kwaajili ya kuongeza tani za uzalishai wa mkonge kutoka tani elfu 37 hadi tanj 120, 000 ifikapo 2023 , zao la mkonge ni moja ya mazoa ambayo mabaki yake na inatoa fursa kubwa kwa vijana kuweza kujitengenezea ajira tunao wataalamu ambao wataenda kwa vijana kuwafundisha vijana namna gani ya kutumia mabaki ya Mkonge kujitengenezea fursa mbalimbali za ajira” amesema Saddi.