NAIROBI, KENYA
OFISA wa Polisi aliyetambuliwa kwa jina la Benny Oduor amefariki dunia baada ya kupigwa jiwe lililokuwa kwenye manati kifuani kaunti ya Kisumu nchini hapa
Tukio hilo limetokea Machi 30, 2023 kufuatiamaandamano yanayoendelea nchini hapa yakiongozwa na kiongozi wa Azimio la Umoja Raila Odinga
Oduor baada ya kupata dhoruba ya kupigwa na jiwe kifuani , alikimbizwa Hospitali ya Aga Khan katika chumba maalum cha wagonjwa mahututi na baada ya muda alipoteza maisha usiku wa Machi 30, 2023.
Kamanda wa Polisi eneo la Nyanza nchini hapa Noah Mwivanda amesema marehemu alirushiwa jiwe hilo kwa manati ya kutengeneza wakati polisi wakikabiliana na waandamanaji