NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
RAIS wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali yake itaendelea kuzingatia utawala wa sheria na kwamba demokrasia ni nyenzo muhimu katika uongozi wake.
Rais Samia ameyasema hayo leo Machi 30, 2023 Ikulu ya Magogoni jijini Dar es Salaam wakati akimkaribisha mgeni wake Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Haris anayefanya ziara ya siku tatu hapa nchini Tanzania.
Rais Dk Samia amesema amejitahidi kuwa na serikali inayozingatia utawala wa sheria na kwamba anamshukuru Rais wa Marekani Joe Biden kupitia mkutano aliyomwalika uliofanyika nchini Marekani kwa njia ya mtandao umetutambua kuwa wanaheshimu demokrasia na utawala wa sheria.
“Ni imani yetu kuwa sio tu ziara hii itakuwa na umuhimu bali itaibua vitu mbalimbali vya ushirikiano baina ya Tanzania na Marekani,”amesema Rais Dk. Samia.