NAIROBI, KENYA
ALIYEKUWA Mgombea Urais nchini Kenya kwa tiketi ya Azimio la Umoja, Raila Odinga ameongeza siku za kuandamana nchini humo.
Awali Azimio la Umoja kupitia kwa Raila Odinga lilitangaza kuwa kutafanyika maandamano kila Jumatatu ya wiki kama ambavyo yalivyofanyika Jumatatu iliyopita
Lakini leo Jumatano, Machi 22, 2023 Azimio la Umoja limemwandikia barua Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Kenya, Japhet Koome kuwa wameongeza siku za maandamano na sasa yatafanyika kila Jumatatu na Alhamisi kuanzia Jumatatu ya Machi 27, 2023.
Tunakutaarifu kuwa tutafanya maandamano kweye kaunti zote 47 za Kenya kila Jumatatu na Alhamisi na tutaanza Jumatatu ijayo ya Machi 27 na Alhamisi ya Machi 30.
Hili sio ombi bali ni taarifa tu kama inavyoelekezwa kwenye ibara ya 37 ya Katiba ya Kenya. Tunaitaka ofisi yako ilinde maandamano yetu na si vinginevyo,” inasomeka barua ya Azimio la Umoja iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Kamati Kuu, Wycliffe Oparanya
Raila Odinga anahamasisha maandamano nchini Kenya wakiitaka serikali kudhibiti mfumuko wa bei.
SOMA ZAIDI:
Eric Omondi, wenzake 17 wafikishwa mahakamani kwa mkusanyiko haramu