NA WALTER MGULUCHUMA, KATAVI
WATU 9 wamepoteza maisha na wengine 25 kujeruhiwa baada ya basi la abiria walilokuwa wakisafiria kupinduka jioni ya leo Machi 06, 2023 eneo la mlima Nkondwe Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi .
Ajali hiyo imehusisha basi aina ya Tata lenye namba za usajili T506 DHH mali ya Tulia Komba lililokuwa likitokea mkoani Kigoma
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi , Ali Makame amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva aliyetajwa kwa jina la Revocatus James.
Ameeleza kuwa kati ya marehemu hao tisa, watano ni wanaume ambapo watoto ni watatu na wanawake ni wanne.
Aidha Kamanda Makame amebainisha kuwa miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya Manispaa ya Mpanda ikisubiri kutambuliwa.