NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA
VIJANA na wanawake nchini wanatarajia kupata ajira Milioni tatu kupitia programu ya Building Better Tomorrow kwa kushiriki Kilimo biashara kupitia mashamba ya pamoja
Akizungumza Jijini Dodoma Waziri wa kilimo Hussein Bashe alipokuwa akitoa taarifa kwa vyombo vya habari alisema Wizara ilitoa tangazo kwa umma kwaajili ya vijana kuwasilisha maombi ili kujiunga na mafunzo ya kilimo biashara katika vituo atamizi.
Waziri Bashe amesema kuwa jumla ya maombi yote yaliyopokelewa ni 20,227 Kati yao wanawake ni 4,722 sawa na asilimia 23.34.
“Wizara imekamilisha taratibu za uchambuzi na kuwapatia vijana 812 watakaoshiriki mafunzo kwa awamu ya kwanza,kati yao wanawake ni 282 sawa na asilimia 34.73 na wanaume 530 sawa na asilimia 65.27 ya waliochaguliwa,
Vijana waliochaguliwa watapata mafunzo kwa kipindi cha miezi minne katika vituo 15 vilivyoandaliwa na watakuwa kuripoti katika vituo watakavyopangiwa tarehe 17 machi mwaka huu bila kukosa,”alisema Waziri Bashe.
Aidha amesema kuwa wakati wote wa mafunzo Serikali itagharamia malazi,chakula na gharama za mafunzo,Aidha vijana watatakiwa kujigharamia usafiri na mahitaji binafsi.
Amefafanua kuwa mkoa wa Dar es salaam umeongoza Kwa kuwa na waombaji wengi wapatao 2,931 sawa na asilimia 14.49 ya maombi yote na mkoa wenye waombaji wachache ni Lindi ambapo jumla ya maombi 109 yalipokelewa sawa na asilimia 0.54.
“Kwa upande wa halmashauri Jiji la Dodoma limeongoza kwa kuwa na waombaji wachache zaidi ni Nyasa ambayo Ina jumla ya waombaji 06 sawa na asilimia 0.03 ya maombi yote,”alisema.