NA MWANDISHI MAALUM, WASHINGTON D.C
RAIS Mstaafu Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na Rais Mstaafu wa Marekani George W. Bush na Dk Condoleezza Rice, Waziri wa Mambo ya Nje Mstaafu wa Marekani, wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Miaka 20 ya Mpango wa Dharura wa Rais wa Kupambana na UKIMWI (PEPFAR), Jijini Washington DC Marekani februari 24, 2023
Katika kuadhimisha miaka hiyo 20 ya mafanikio ya PEPFAR, licha ya kwamba Mpango huo unatekelezwa katika nchi mbalimbali Afrika na Asia, Taasisi ya George Bush Foundation wameamua kumualika Dk Kikwete kwa kutambua mchango wake mkubwa katika kuufanya Mpango huo kuwa na mafanikio.
Tanzania imekua ni nchi ya kupigiwa mfano kwa namna walivyofanya jitihada za kupambana na ugonjwa wa Ukimwi kwa jitihada zao wenyewe kama nchi na kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa kimataifa kama vile PEPFAR.