NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Agosti 25, 2025 ni mgeni rasmi katika kongamano la kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima inayofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Lengo kuu la kongamano hilo ni kuhakikisha kuwa elimu ya watu wazima inakuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kiteknolojia kwa nchini. Pia ni jukwaa la kubadilishana uzoefu, matokeo ya tafiti na mbinu bora zinazoweza kuendeleza ubunifu katika utoaji wa elimu ya watu wazima.
Kongamano hilo linalofanyika kuanzia leo tarehe Agosti 25, 2025 hadi Agosti 27, 2025 lina kaulimbiu isemayo Elimu Bila Ukomo kwa Maendeleo Endelevu.”