*AWAPONGEZA WMA KWA UTENDAJI KAZI MZURI
*NI BAADA YA KUTEMBELEA BANDA LAO MAONESHO YA NANENANE
NA MWANDISHI WETU, DODOMA
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi amewataka Watendaji wa Wakala wa Vipimo (WMA)kuendelea kuchapa kazi kwa bidii ili kuwalinda walaji katika sekta zote nchini wakiwemo wakulima kupitia jukumu lao kuu la uhakiki wa vipimo.
Aidha amewapongeza watendaji wa WMA kwa utendaji kazi wake wanaoufanya.
Profesa Kabudi ameyasema haya wakati alipotembelea Banda la Wakala wa Vipimo katika Maonesho ya NaneNane mkoani Dodoma.
Pamoja na mambo mengine
Waziri Kabudi amesema WMA ni miongoni mwa Taasisi muhimu za Serikali zinazogusa maisha ya wananchi moja kwa moja.