NA MWANDISHI WETU
AlLOYCE Tendewa Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) jina lake limepitishwa kwenda kwa wajumbe kuwania nafasi ya Ubunge.
Tendewa aliyekuwa msaidizi wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu Edward Lowassa ameonesha nia yake kuwa Mbunge wa Kilombero.
Kada huyo jina lake limo kati ya majina manane yaliyopitishwa na kamati kuu ya CCM na kutangazwa na Katibu wa Uenezi, Itikadi na Mafunzo CPA Amos Makalla.
Tendewa ni mmoja wa Wagombea wachache ambaye anaishi jimboni humo kutofautiana na wengi ambao wanaishi nje ya Jimbo la Kilombero.