NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
MKUU wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda, ametoa wito kwa Wafanyabiashara kote nchini kuchangamkia fursa za kibiashara zinazotolewa na Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA).
DC Mapunda ametoa wito huo leo Julai 03,2025 alipotembelea banda la TCCIA kwenye Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ( Sabasaba) jijini Dar es Salaam .
Pamoja na kutoa witi huo DC Mapunda alipata wasaa wa kupokea maelezo kuhusu shughuli na huduma mbalimbali zinazotolewa na TCCIA katika kuendeleza sekta binafsi.
DC Mapunda alielezwa kuhusu mafanikio ya utoaji wa Cheti cha Uasili wa bidhaa kwa njia ya kidijitali, ambao sasa unarahisisha sana mchakato wa biashara kwa wazalishaji na wauzaji wa bidhaa nje ya nchi.
Aidha DC Mapunda alifahamishwa kuhusu uwakilishi wa TCCIA katika Mabaraza ya Biashara, yanayojadili masuala mtambuka ya biashara kati ya sekta binafsi na serikali.
Baada ya kupokea maelezo hayo huku akiwa na furaha kwa mafanikio hayo, DC Mapunda alisema “TCCIA mnatoa huduma ya maana sana kwa wafanyabiashara wetu
” Mageuzi haya ya kidijitali kwenye vyeti vya uasili si tu yanapunguza muda na gharama, bali pia yanaongeza ushindani wa bidhaa zetu kimataifa” alisema na kuongeza
” Hili la kuwawakilisha wafanyabiashara kwenye mabaraza ya maamuzi ni jambo la msingi sana tunawapongeza”
TCCIA inaendelea kushirikiana na Serikali na Sekta Binafsi kuimarisha mazingira ya biashara.