NA MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAM
IMEELEZWA kuwa matumizi ya asali ni hatari kuliko sukari.
Hatari hii inakuja kutokana na kubainika kwamba asali inaongeza uzito zaidi ya sukari.
Haya yanabainishwa na Ofisa Lishe na Muuguzi Mbobezi Kitengo cha Wagonjwa Mahututi kutoka Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI), Zainabu Tindi .
Tindi anayasema haya wakati wa mahojiano maalumu baina yake na Demokrasia kwenye banda la MOI lililopo katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Tindi amesema asali ina kiwango kikinwa cha kalorizi kuliko Adam ambapo kijiko kimoja cha asali kina kalorizi 64 na sukari ina kalorizi 45
” Kipi ni kitamu Kati ya asali na sukari…jibu ni asali hivyo kwa mantiki hiyo unaweza kujionea utofauti mkubwa wa kalorizi uliopo baina sukari na asali hivyo basi nashauri wanaotaka kupunguza uzito kuacha kabisa matumizi ya asali “amesisitiza Ofisa huyo
Aidha alishauri si vyema watoto wadogo NA wazee wakajihusisha na matumizi ya asali kwa mustakabali wa afya zao.
” Watu wanadanganyana sana juu ya kwamba asali ni bora na ni mandala wa sukari lakini kimsingi sio kweli , kikubwa ni Jamii kwa ujumla kufuata kanuni za lishe bora ili kuepukana na magonjwa,na uzito uliopitiliza.”amehitimisha Tindi