NA SHAMIMU NYAKI,KILIMANJARO
WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Damas Ndumbaro leo Februari 24, amewasili Moshi mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya msimu wa 22 wa Mbio za kimataifa za Kili Marathon zitakazofanyika mapema februari 25, 2024 katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika.
Baada ya kuwasili Ndumbaro amepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Kisare Makori na waandaji wa mbio hizo kampuni ya Kilimanjaro Marathon Limited na Executive Solution ambao wamemhakikishia kuwa maadalizi ya mbio hizo yamekamilika.
Mbio hizo zitahusisha wakimbiaji kutoka nchi zaidi ya 50 duniani ikiwemo Marekani, Uingereza, Uholanzi, Ufaransa Kenya, Uganda na Afrika Kusini kwa wakimbiaji wa umbali wa Kilometa 42, Kilometa 21, Kilometa 10 na Kilometa 5.