NA MWANDISHI WETU,BANGKOK,THAILAND
GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba, ametunukiwa tuzo maalum ya Magavana wa Benki Kuu waliopata Daraja A kwa mwaka 2026 na taasisi ya kimataifa ya Global Finance.
Gavana Tutuba ametunukiwa tuzo hiyo kwa kutambua mchango wake katika usimamizi wa sera ya fedha, sekta ya fedha na kukuza huduma jumuishi za fedha.
Tuzo hiyo imetolewa Jumamosi Oktoba 17,2026 jijini Bangkok, nchini Thailand, wakati wa mikutano ya mwaka ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) na Kundi la Benki ya Dunia (World Bank Group).
Imeelezwa kuwa tuzo hiyo ni heshima kubwa kwa Benki Kuu na Taifa kwa ujumla.
Pia tuzo hiyo ina akisi mchango wa BoT katika kusimamia sera ya fedha na kuendeleza sekta ya fedha iliyo imara na jumuishi.

