NA MWANDISHI WETU, LISBON, URENO

(DIB), Isack Kihwili (wa tatu kutoka kushoto)
akishiriki katika kikao jijini Lisbon, Ureno
ambako unafanyika Mkutano Mkuu wa
Mwaka wa Jumuiya ya Kimataifa ya Taasisi za
Bima ya Amana (IADI-AGM). Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Umma na Itifaki wa DIB, Lwaga Mwambande. Mikutano ya IADI ambayo ilianza Novemba 24, inatarajiwa kuhitimishwa Novemba 28,2025.
BODI ya Bima ya Amana (DIB) imetambuliwa katika mkutano wa kimataifa wa taasisi za bima ya amana kwa kuanza kutekeleza jukumu la kupunguza hasara kwa Benki badala ya kusubiri kulipa fidia benki zinapoanguka.
DIB imetambuliwa katika taarifa iliyotolewa katika kikao cha Kamati ya Kanda ya Afrika (ARC) kama sehemu ya Mkutano Mkuu wa mwaka wa 24 wa Jumuiya ya Kimataifa ya Taasisi za Bima ya Amana (IADI-ARC) unaoendelea jijini Lisbon, Ureno.

Mwenyekiti wa Kanda ya Afrika ya Taasisi za Bima
ya Amana (ARC, Dk. Julia Oyet, kutoka Mfuko wa Bima ya
Amana Uganda (DPF) na Katibu Mstaafu wa
ARC, Olivier Musengimana kutoka
Rwanda wanaoshiriki katika Mkutano Mk
uu wa Mwaka wa 24 wa Jumuiya ya Kimataifa ya Taasisi za Bima y
a Amana (IADI) unaoendelea jijini Li
sbon, Ureno.
Jukumu hili limeanza kutekelezwa na DIB Julai 2025 huku lengo ni kuhakikisha benki au taasisi ya fedha inayopitia changamoto katika biashara yake kusaidiwa ili irudi katika hali ya kawaida badala ya kusubiri hadi benki au taasisi hiyo ya fedha ife na kulipa fidia ilihali Kupunguza hasara kunaweza kuwa nafuu zaidi kuliko kama taasisi kama hiyo ikaachwa hadi ianguke.
Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa DIB Isack Kihwili alipata fursa ya kupiga picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Kanda ya Afrika ya Taasisi za Bima ya Amana (ARC), Dk Julia Oyet (katikati) Uganda (DPF) na katibu mstaafu wa ARC, Olivier Musengimana kutoka Rwanda.

