NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
MAMBO yanazidi kunoga katika mnada wa Piku Africa, ambapo watu watatu kutoka maeneo tofauti jijini Dar es Salaam wamejinyakulia bidhaa zenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni tatu.
Miongoni mwa washindi hao ni Sara Kyando (23), mkazi wa Kinondoni na mfanyakazi wa kampuni ya moja inayojishughulisha na masuala ya elimu ambaye amejishindia simu Janja aina ya Samsung A06 yenye thamani ya Sh. 250,000.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Sarah amesema aligundua kuhusu Piku kupitia mtandao wa Instagram, na baada ya kuona washindi wengine, alihamasika kushiriki.
“Nilijaribu kucheza na kufanikiwa kushinda. Nawashauri vijana wenzangu watumie vizuri mitandao ya kijamii kwa kushiriki katika minada kama hii, kwani inaweza kuwasaidia kupata bidhaa bora na kwa gharama nafuu,” amesema Sara kwa furaha.
Mshindi mwingine ni Gloria Emil (28), mkazi wa Tegeta, ambaye amejinyakulia simu janja aina ya Samsung A06, amesema amefurahia zawadi hiyo kwa kuwa simu yake ya awali ilikuwa imeharibika.
“Kupitia simu hii mpya ya Piku nitakuwa na mawasiliano bora zaidi na ndugu zangu pamoja na wateja wangu.nawashukuru Piku kwa urahisi huu, kwani wamenisaidia katika kufanikisha biashara zangu,” amesema Emil
Kwa upande wake, Obeid Joshua (20) mkazi wa Mbezi, ambaye amejinyakulia televisheni aina ya LG pamoja na router ya Airtel yenye bando la mwaka mzima, vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 2.4, amesema Piku ni mnada wa kipekee na unaowavutia watu wengi hasa vijana.
Joshua amesema aliifahamu Piku kupitia mitandao ya kijamii baada ya kuona tangazo la mshindi wa bodaboda mpya aina ya TVS, jambo lililomhamasisha kujaribu bahati yake na hatimaye amejinyakulia bidhaa nzuri na yenye ubora.
“Najisikia furaha sana kushinda bidhaa hizi. Piku ni ya kweli kabisa, siyo janja janja. Nawashauri vijana wenzangu wasisite kushiriki. Hata kama hukushinda mara ya kwanza, endelea kujaribu kwa sababu bidhaa ni nyingi na kila siku kuna nafasi mpya ya kushinda,” amesema
Kwa upande wake, Balozi wa Piku Africa, Saphiness Rabieth, amesema kuwa jukwaa la Piku limejipanga vizuri kuhakikisha washiriki wote wanapata bidhaa za kisasa na zenye bora wa hali ya juu.
“Tunatoa zawadi nyingi kila siku, ikiwemo simu janja aina ya Samsung A06 kila baada ya siku tatu. Wateja wanachotakiwa kufanya ni kupakua App ya Piku kwenye Play Store kwa watumiaji wa Android au App Store kwa wenye iPhone. Tiketi za mnada zetu zinapatikana kuanzia Sh. 1,000 hadi 100,000,” amesema Rabieth
Kwa ujumla, washiriki wa Piku Africa wanaendelea kuthibitisha kuwa jukwaa hili ni la kweli, lenye uwazi na fursa halisi za kujishindia bidhaa bora kwa dau dogo na la kipekee.