NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
JUKWAA la kidijitali la PIKU linalojulikana kwa kufanya minada ya kipekee na yenye ushindani wa hali ya juu, limetangaza kuja na bidhaa mpya na za kuvutia zitakazoshindaniwa na washiriki wake wote.
Kwa mara ya kwanza washiriki wa mnada wa PIKU watapata nafasi ya kushindania bidhaa zenye thamani kubwa ambazo ni gari, pikipiki, seti ya dhahabu x, simu janja, televisheni pamoja na manukato ya gharama (pafyumu).
Akizungumza na Waandishi wa Habari Meneja wa Habari na Mawasiliano PIKU, Barnabas Mbunda amesema kila baada ya siku 112 watafunga mwaka kwa mtu kujishindia gari aina ya Toyota Raum lenye bima ya mwaka mzima na kadi ya mafuta vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Milioni 30.
Amesema kwenye mgodi wa Piku, baada ya siku 56, seti ya dhahabu safi yenye thamani ya Milioni sita itatolewa kwa atakayeibuka mshindi kwa kuweka dau dogo na la kipekee na kwamba mshindi wa mnada huo atakwenda mwenyewe dukani kuchagua seti anayotaka.
“Kwenye Zigo la Piku hapa baada ya siku 28, mtu atakayeweka dau dogo na la kipekee atajipatia Pikipiki ya TVS mpya kabisa ikiwa na helmeti, kiakisi mwanga, kadi ya mafuta ya miezi sita na bima.Thamani ya zigo hilo ni Sh. Milioni nne,” amesema.
Hata hivyo Mbunda amesema kwenye Combo la Piku, kila baada ya siku 14 zitatolewa saa ya kisasa, manukato ya gharama vitu hivyo vyote vikiwa na thamani ya Sh. Milioni moja na kuongeza kuwa katika combo hilo kutakuwa pia na Televisheni ya LG inchi 55 na Airtel Router iliyolipiwa mwaka mzima, vyote hivyo vikiwa na thamani ya Milioni 2.4.
Ameendelea kusema kuwa katika bando la wiki la mnada huo mtu atakayeweka daud ogo na la kipekee atajinyakulia simu janja, outdoor speaker vyote vikiwa na thamani ya Sh. 500,000.
Mbunda amesema hatua ya uwekaji wa bidhaa hizo katika mnada wake ni sehemu ya mkakati wa Piku kupanua wigo wa huduma zake na kuhakikisha kila mshiriki anapata fursa ya kushindania bidhaa kubwa zinazobadilisha maisha yake.
Amesema vijana na watu wazima kuanzia miaka 18 na kuendelea wanaruhusiwa kushiriki katika minada ya PIKU kwa kupakua App ya jukwaa hilo ambapo kwenye simu za adroid unaingia kwenye ‘play store’ na Iphone kwenye App Store.
“Washiriki wanaweza kununua tiketi kwa bei nafuu kuanzia Sh.1,000 kwa tiketi 10, sh. 5,000 kwa tiketi 50, sh. 10,000 kwa tiketi 100, na kuendelea hadi sh 100,000, ambapo nafasi ya ushindi huwa kubwa zaidi,”. amesema Mbunda
Hata hivyo amesema mbali na bidhaa hizo tayari mnada wa Piku umeshatoa mshindi ambapo mtu wa kwanza ni Mjasiriamali Sabri Hamis mwenye makazi yake Zanzibar aliyejishindia vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Milioni tano.
Mbali na Sabri mshindi mwingine ni Jenipher Ayubu aliyejishindia friji la milango miwili (LG), mashine ya kufulia (LG), Microwave, Food Processor, Jiko la Umeme na Seti nzima ya vyombo vya jikoni vitu vyote hivyo vikiwa na thamani ya sh. Milioni nne.