NA MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAM
BANDARI ya Dar es Salaam imefunga mwaka wa fedha wa 2024/25 kwa kuhudumia tani milioni 27.7, kutoka tani milioni 18 za mwaka 2021/22 na tani zaidi ya milioni nne kuliko mwaka 2023/2024 ambapo ilikuwa na tani milioni 23.69.
Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam,Abed Gallus.
Gallus alimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TPA Plasduce Mbossa, amesema kukua kwa asilimia 15 kwa mwaka ni jambo kubwa ambalo halikuwahi kutokea tangu kuanzishwa kwa Bandari hiyo.
“Kwa wamiliki wa mizigo na wasafirishaji wamepata nafuu na mafanikio makubwa ambayo hayakutarajiwa,” amesema na kuongeza kuwa
Chini ya mradi wa DMGP, mlango wa kuingilia Meli Bandarini na kina cha Bandari kimeongezeka na kuimarika na kwa sasa kumekuwa na urahisi mkubwa wa kupokea mizigo na kuondolewa Bandarini haraka.“
Mwanzo meli moja ya Kontena ilikuwa inachukua zaidi ya siku 10 kushushwa mzigo wake bandarini lakini sasa ni ndani ya siku tatu tu,”amesema Gallus.”
Amesema Bandari ya Dar es Salaam ndiyo kubwa zaidi nchini Tanzania, ikiwa inahudumia zaidi ya asilimia 95 ya Biashara za kimataifa” ameongeza Mkurugenzi huyo.
Amesema Kwa kuzingatia kukuwa kwa kiwango hicho, mapato yameongezeka na hivyo kuifanya nchi kupata faida kubwa, kwa sababu ya kuwa na uwezo wa kupokea mizigo mingi kwa wakati mmoja.
Gallus aliwasihi Wateja na Wadau kuendelea kuitumia Bandari ya Dar es Salaam, akisisitiza juu ya huduma zenye ufanisi mkubwa na uwezo wa juu.