NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
JUMUIYA ya Wafanyabishara (JWT), imesema Serikali haina lengo la kuwakomoa au kuwafukuza wafanyabishara wageni nchini, bali kulinda uchumi wa ndani kwa kuweka sheria za dhidi ya shughuli 13 za biashara zinazotakiwa kufanywa na wazawa pekee.
Mwenyekiti wa JWT, Hamis Livembe, aliyasema hayo jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu malalamiko ya wanaodai serikali kuwazuia wageni kufanya biashara nchini.
Alisema Serikali imeandaa sheria hiyo maalum ya kutenga baadhi shughuli zikiwamo biashara ndogo ndogo zinazoweza kufanywa na Watanzania kutofanywa na wageni ili kulinda soko la ajira la ndani.
Livembe alisema lengo la Serikali ni kulinda ajira za wazawa kwasababu haina uwezo wa kuajiri Watanzania wote hivyo sheria hiyo inaweka ukuta wa kuwalinda uchumi wa watu wake.
Alisema kuwapo kwa sheria hiyo kutasaidia kuondoa migogoro kati ya wafanyabishara wazawa na wageni nchini iliyokuwa ikiendelea mara kwa mara.
“Kama unakumbuka jambo hili lilizungumzwa na Rais Samia Suluhu Hassan, pale Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati akiwapongeza wale waliokoa watu walikutwa na majanga ya kuporomoka kwa jengo la Kariakoo na tope la Mlima Hanang’ mkoani Manyara.
“Pale Rais Samia, alipokea kero au maoni ya mmoja akilalamikia fujo za wageni wanaofanya biashara Kariakoo na yeye Rais Samia alithibitisha kuona wafanyabishara wakilumbana,” alisema Livembe.
Aliendelea kusema, Rais Samia alimwagiza Waziri wa Viwanda na Biashara, Selemani Jafo, kuunda Tume ya kuchunguza raia wa kigeni wanaofanya biashara Soko la Kariakoo.
“Tunaishukuru sana serikali kwa kulinda maslahi ya wazawa ambao ni wafanyabishara wadogo, badala ya kuwaacha wageni kutawala kila kitu. Sisi tunamshukuru Rais Samia na Waziri wa Viwanda na Biashara, Selemani Jafo, kwa kazi hii kubwa iliyofanyika,”
Alisema JWT walipeleka mapendekezo 50 ya aina shughuli za kuzuia kupeleka mapendekezo 50 na zikafanyiwa upembuzi yakinifu na kupatikana 15 ambazo zinatakiwa tu kufanywa na Watanzania na nyingine zote zifanywe na wageni na wazawa.
“Tunaishukuru sana serikali kwa kulinda maslahi ya wazawa ambao ni wafanyabishara wadogo badala ya kuwaacha wageni kutawala kila kitu. Sisi tunamshukuru Rais Samia na Waziri wa Viwanda na Biashara, Selemani Jafo, kwa kazi hii kubwa iliyofanyika,” aliyofanyika.
Aidha, alisema wapo baadhi wanaolalamikia kuwa faini ya Sh. milioni 10 na adhabu ya kifungo cha miezi sita, jela kwa mfanyabiashara raia wa kigeni atakayekiuka sheria hiyo iliyowekwa kuwa ni ndogo, inatosha na ikionekana haitawaumiza watapeleka mapendekezo ya kufanyika marekebisho mengine.
Kati ya shughuli zilizopigwa marufuku ni uuzaji wa bidhaa kwa rejareja, huduma za saluni, uhamishaji wa fedha kwa njia ya simu na uanzishaji au uendeshaji wa vituo vya redio na Televisheni.
Aidha, huduma za uongozaji watalii, uendeshaji wa mashine za kamari nje ya kasino rasmi na kumiliki viwanda vidogo pia zimewekwa kwenye orodha hiyo.
Shughuli nyingine zilizozuiwa ni biashara ya uwakala wa fedha, udalali katika sekta ya ardhi na biashara, matengenezo ya simu na vifaa vya kielektroniki, huduma za usafi wa nyumbani na maofisini, huduma za forodha na usafirishaji, pamoja na uchimbaji mdogo wa madini. Pia, wageni hawataruhusiwa kununua mazao moja kwa moja kutoka shambani.
Adhabu kwa watakaokiuka ni faini ya hadi Sh. milioni 10, kufutiwa visa na vibali vya ukaazi, au kifungo cha hadi miezi sita.
Kwa Watanzania watakaobainika kuwasaidia wageni kuendesha biashara hizo kwa mgongo wa nyuma, adhabu ni faini ya hadi Sh. milioni 5 au kifungo cha miezi mitatu.