NA MWANDISHI MAALUM,BELARUS
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa Julai 21, 2025 amewasili nchini Belarus kuanza ziara ya kikazi nchini humo ambapo alipokelewa na Naibu Waziri Mkuu wa Beralus, Viktor Karankevich kwenye Uwanja wa Ndege wa Kinsk.
Katika ziara hiyo, Majaliwa ameambatana na Balozi wa Tanzania Urusi na Belarusi, Frederick Ibrahim Kibuta , Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais, Kazi , Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Shariff Ali Shariff na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Cosato Chumi.