NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imetoa gawio la Sh. Bilioni 10.5/- kwa serikali kwa mwaka 2025,kutoka Sh.Bilioni 1.3/- ya mwaka jana.
Gawio hilo limetolewa leo Juni 10,2025 Ikulu jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Rais Samia Suluhu Hassan katika hafla ya kupokea gawio na michango kutoka kwa taasisi na mashirika ya umma.
Akitangaza magawio hayo Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu amesema
“Nao Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) wametoa Bilioni 10 mwaka huu kutoka Bilioni 1.3 ambazo walitoa mwaka jana”
Amesema gawio zinatokana pia na kuimarisha Bodi za wakurugenzi kwani idadi ya taasisi na mashirika yasiyokuwa na bodi za wakurugenzi imepungua kutoka taasisi 52 mwaka 2019/2020 hadi kufikia taasisi 28 mwaka huu ikiwa ni ufanisi wa asilimia 46.
Mchechu amesema kumekuwa na kuimarika kifedha kwa mashirika ya umma yaliyokuwa na mitaji hasi na yaliyokuwa yanapata hasara mfululizo, ambapo sasa yameweza kuondokana na utegemezi wa ruzuku ya Serikali na kufanikiwa kutoa gawio.