NA MWANDISHI MAALUM,ETHIOPIA
RAIS Mstaafu wa Tanzania,Jakaya Mrisho Kikwete ametembea Qasir la Taifa la Ethiopia ambalo lilikuwa makazi ya Mfalme Haile Selassie.
Kikwete alitembelea Qasir hilo kufuatia maombi ya Waziri Mkuu wa Ethiopia, Dk.Abiy Ahmed ambapo walikutana jijini Addis Ababa Aprili 11, 2025 kwa ajili ya kuwasilisha Ujumbe Maalum wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Qasir hilo ambalo kwa sasa limegeuzwa kuwa Makumbusho ni eneo muhimu kwa kuwa limekusanya urithi wa utamaduni wa Ethiopia ambao kimsingi bado haujatumika ipasavyo kwa faida ya wananchi wa Taifa hilo.
Awali, Kikwete alikutana na wafanyakazi wa ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia wakiongozwa na Balozi Innocent Shiyo na kuwasihi kushikamana na utamaduni wa Tanzania ambao miaka yote umekuwa ukihamasisha umoja barani Afrika.