NA MWANDISHI WETU,DODOMA
TUZO Maalumu iliyotolewa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolph Mkenda kuhusu maono na mchango wake kwenye Sekta ya Elimu ilitengenezwa na Kituo Cha Jemolojia Tanzania ( TGC) kilicho chini ya Wizara ya Madini.
Kituo hiki kilichopo jijini Arusha, kinatoa mafunzo ya Uongezaji Thamani Madini ya Vito na miamba.
Tuzo hiyo ilitengenezwa kutumia madini ya Zoisite yanayopatikana nchini
Zoisite ni Madini ya kuvutia yanayopatikana kama mwamba mama wa Madini ya Ruby, yakitengeneza mchanganyiko maarufu wa Ruby-Zoisite (Anyolite).
Mchanganyiko huu wa kipekee wa Zoisite ya kijani na ruby nyekundu huvutia kwa utofauti wake wa asili na uzuri wake wa kipekee.
Kituo cha Jiolojia cha Tanzania (TGC) kilitambua rasmi na kuainisha mwamba huu wa thamani, ukionesha umuhimu wake katika dunia ya madini.
Tuzo hiyo ilitolewa wakati wa Hafla ya Uzinduzi wa Sera ya Elimu na Mafunzo kwa Mwaka 2014 toleo la 2023 iliyofanyika Februari 1, 2025.