NA ANDREA NGOBOLE,ARUSHA
RAIS Dk.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufungua Kongamano la 42 la Chama cha Madaktari wa Wanyama Nchini , litakalohusisha zaidi ya Wadau 2000 wa Wanyama kutoka Nchi za Jumuiya ya Madola, katika Hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha mapema kesho Desemba 3, 2024
Kongamano hilo litafanyika kwa siku tatu kuanzia 3 hadi 5, Desemba 2024 limeandaliwa na Chama cha Kitaaluma cha Madaktari wa Wanyama Nchini Tanzania (TVA)
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mwenyekiti wa Chama hicho, Profesa Esron Karimuribo amesema Kongamano hilo la kisayansi litakalofunguliwa na Rais Samia lina umuhimu mkubwa kwa nchi na wananchi kwani ndilo linaloangazia namna bora ya kuzuia, kudhibiti na kutokomeza magonjwa ya Wanyama kuimarisha moja ya walaji wa Wanyama duniani.
Aidha, litaangazia maeneo muhimu ya kuishauri Serikali jinsi ya kuboresha Sekta ya Mifugo nchini ili kufanya biashara nzuri ya mifugo Kitaifa na Kimataifa kwa kukuza Uchumi wa Wafugaji na kuongeza pato la Taifa kwa ujumla.
Amesema kuwa Kongamano hilo litashirikisha wadau wapatao 2000 ambao ni Wanachama wa Chama cha Madaktari wa Wanyama Nchini, Madaktari wasaidizi wa wanyama, Madaktari Wastaafu, wazalishaji wa chanjo za Wanyama, na Wataalamu wa Afya za Wanyama kutoka nchi zinazounda Jumuiya ya Madola.
Katibu wa Chama hicho Caroline Uronu amesema Chama hicho kilianzishwa mwaka 1982 na kila mwaka kimekuwa kikifanya Kongamano la Kisayansi na mwaka huu litakuwa Kongamano la 42 tangu kuanzishwa kwa chama hicho ambapo moja ya majukumu ya Chama hicho ni kupaza sauti za ustawi wa Madaktari wa Wanyama nchini, kujenga mahusiano ya kitaaluma ya madaktari wa Wanyama wa Kitaifa na Kimataifa na pia kujenga Jukwaa linalosaidia kujenga hoja mbalimbali za maendeleo ya Chama na Wanachama wa Chama hicho.
Awali akizungumzia Sekta ya Mifugo nchini Tanzania, Profesa Gabriel Shirima Kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) ambaye pia ni Daktari wa mifugo na Mwanachama wa chama cha (TVA) amesema sekta ya mifugo ina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi nchini, pia hutoa lishe bora kwa wananchi kwani vitamini ya Wanyama ndiyo ghali zaidi Rais Dk. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufungua Kongamano la 42 la Chama cha Madaktari wa Wanyama nchini , litakalohusisha zaidi ya Wadau 2000 wa Wanyama kutoka nchi za Jumuiya ya Madola, katika Hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha mapema kesho Desemba 3,2024
Kongamano hilo litafanyika kwa siku tatu kuanzia 3 hadi 5, Desemba 2024 limeandaliwa na Chama cha Kitaaluma cha Madaktari wa Wanyama Nchini Tanzania (TVA)
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mwenyekiti wa Chama hicho, Profesa Esron Karimuribo amesema Kongamano hilo la kisayansi litakalofunguliwa na Rais Samia lina umuhimu mkubwa kwa nchi na wananchi kwani ndilo linaloangazia namna bora ya kuzuia, kudhibiti na kutokomeza magonjwa ya Wanyama kuimarisha moja ya walaji wa Wanyama duniani.
Aidha litaangazia maeneo muhimu ya kuishauri Serikali jinsi ya kuboresha Sekta ya Mifugo nchini ili kufanya biashara nzuri ya mifugo Kitaifa na Kimataifa kwa kukuza Uchumi wa Wafugaji na kuongeza Pato la Taifa.
Amesema kuwa Kongamano hilo litashirikisha wadau wapatao 2000 ambao ni Wanachama wa Chama cha Madaktari wa Wanyama nchini, Madaktari wasaidizi wa wanyama, Madaktari Wastaafu, wazalishaji wa chanjo za Wanyama, na Wataalamu wa Afya za Wanyama kutoka nchi zinazounda Jumuiya ya Madola.
Katibu wa Chama hicho Caroline Uronu amesema Chama hicho kilianzishwa mwaka 1982 na kila mwaka kimekuwa kikifanya Kongamano la Kisayansi na mwaka huu litakuwa Kongamano la 42 tangu kuanzishwa kwa chama hicho ambapo moja ya majukumu ya Chama hicho ni kupaza sauti za ustawi wa Madaktari wa Wanyama nchini, kujenga mahusiano ya kitaaluma ya Madaktari wa Wanyama wa Kitaifa na Kimataifa na pia kujenga Jukwaa linalosaidia kujenga hoja mbalimbali za maendeleo ya Chama na Wanachama wa Chama hicho.
Awali akizungumzia Sekta ya Mifugo nchini Tanzania, Profesa Gabriel Shirima Kutoka Chuo cha Nelson Mandele ambaye pia ni Daktari wa mifugo na Mwanachama wa chama cha (TVA) amesema sekta ya mifugo ina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi nchini, pia hutoa lishe bora kwa wananchi kwani vitamini ya Wanyama ndiyo ghali zaidi duniani, huongeza mapato ya familia na ajira kwa vijana.
Amesema Sekta hiyo inatoa pia malighafi kwenye viwanda vya ndani, kupata fedha za kigeni kwa kuuza nyama nje ya nchi na mbolea ya asili ambayo inafaa sana kwa kuongeza mazao shambani duniani, huongeza mapato ya familia na ajira kwa vijana.
Amesema Sekta hiyo inatoa pia malighafi kwenye viwanda vya ndani, kupata fedha za kigeni kwa kuuza nyama nje ya nchi na mbolea ya asili ambayo inafaa sana kwa kuongeza mazao shambani.