NA MWANDISHI WETU, TANGA
TAKUKURU Mkoa wa Tanga imeongeza ufanisi wa ukusanyaji mapato ya Sh. Bilioni 1.9 yatokanayo na ada za Lesseni za Biashara, Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni na Ushuru wa Huduma.
Hii imetokana na hatua zilizochukuliwa baada ya kubaini zaidi ya asilimia 64 ya wafanyabiashara kutokuwa na lesseni za biashara na asilimia 90 kutolipa Ushuru wa Huduma na Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni Jijini Tanga.
Pia umefanyika ufuatiliaji wa miradi 41 yenye thamani ya zaidi ya Sh. Bilioni 19.7
Hayo yamesemwa na Mkuu wa TAKUKURU (M) Tanga Ramadhani Ndwatah wakati akiwasilisha Taarifa ya Utendaji Kazi ya Mkoa wa Tanga kwa kipindi cha Mwezi Julai hadi Septemba 2024.