NA ASHRACK MIRAJI,TANGA
MATUNDA ya Uwekezaji wa Bandari ya Tanga wa Sh.Bilioni 429 uliofanywa na Serikali umeanza kulipa kutokana na maboresho makubwa na hivyo kuwezesha ongezeko kubwa la idadi ya meli zinazopitisha shehena kutoka meli 197 kwa mwaka 2022/2023 hadi kufikia meli 307 kwa mwaka 2023/2024
Hayo yalisemwa na Meneja wa Bandari ya Tanga, Mrisha Masoud wakati akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kuipokea meli ya XINHAITONG 50 iliyotoka nchini China moja kwa moja kuleta shehena ya magari kupitia kampuni ya Meli ya SeaFront Shipping Services Limited (SSS).
Alisema ujio wa meli hizo kushusha magari katika Bandari hiyo inadhihirisha kwamba ufanisi mkubwa katika shughuli za kupakia na kupakua zimeimarika kutokana na maboresho hayo makubwa.
“Lakini niseme kwamba maboresho haya pia yameleta ongezeko kubwa la ajira na hadi sasa idadi ya makampuni ya wakala wa usafirishaji katika bandari yameongezeka kutoka 32 hadi 132”Alisema
Akizungumzia kuhusu ongezeko la mapato katika Bandari hiyo alisema kwamba yameongezeka ambapo kwa mwaka wa fedha 2022/2023, Bandari ilikusanya mapato ya Sh.Bilioni 16 lakini kwa mwaka 2023/2024 mapato hayo yameongezeka hadi Sh.Bilioni 18.6 ikiwa ni ongezeko la asilimia 74.1.
“Ongezeko hilo la mapato linatokana na maboresho yaliyofanyika katika bandari ya Tanga,na ni muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa nchi kwa ujumla “Alisema
Alisema kwamba maboresho haya yanaonesha jinsi uwekezaji katika miundombinu unavyoweza kuleta matokeo chanya kwa jamii na uchumi wa Taifa.
Hata hivyo alisema Serikali inaendelea na juhudi za kuboresha sekta ya usafirishaji ili kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa kitovu cha biashara katika eneo la Afrika Mashariki.
Awali akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA,Ofisa Uhusiano wa TPA nchini Enock Bwigane amesema wan mshukuru mdau wa kampuni ya Sea Front ambaye amefanikisha kuwasili kwa meli hiyo iliyobeba shehena mchanganyiko yakiwemo magari zaidi ya 350.
Bwigane alisema kwamba asilimia kubwa ya shehena hiyo inaelekea nje ya nchi na kuwepo kwa meli hiyo ambayo inahudumiwa kwa saa 48 tangu ifike leo alfariji inafikisha meli idadi ya meli 12 ambazo zimehudumiwa na mteja wao Kampuni ya Sea Front Shipping.
Alisema kwamba mteja wao huyo alikuwa akifanya huduma za kibandari katika Bandari ya Dar lakini kutokana ana uwekezaji uliofanywa na Serikali wa Bilioni 429 .1 kwa awamu zote mbili kuboresha bandari ya Tanga umepelekea meli kubwa nyingi kwa shehena tofaui kuhudumiwa katika Bandari ya Tanga.
“Huyu ni mteja mojawapo alileta meli kutoka nchini China na ambapo meli hii imefikisha idadi ya meli 12 ambazo zimeshuhudumiwa na tunapoongelea ufanisi wa mapato katika Bandari ya Tanga tunajivunia”alisema
Alisema robo ya kwanza ya Julai Mosi hadi Septemba 30 mwaka huu Bandari hiyo ilikusanya Bilioni 18.6 na Bilioni 8 katika mapato hayo zimetokana na mteja huyo ambaye amekwisha kuwezesha ujio wa meli 12 katika Bandari hiyo.
“Tunamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa maamuzi yake ya kufanya maboresho katika Bandari zote nchini ikiwemo Bandari ya Tanga ambapouwekezaji mkubwa uliofanyika umesaidia kuongeza ufanisi katika Bandari na mapato yameongezeka na huduma ya shehena zimeongezeka kila mwaka ukiangalia kwa miaka miwili iliyopita”alisema
Alisema shehena hiyo imeongezeka kutoka kuhudumia shehena tani 800,000 na sasa wana Milioni 1.5 na mwaka huu wanatarajia kuhudumia shehena tani Milioni 1.4 katika robo ya kwanza na wameshahudumia shehena tani laki 3.3 .
Aidha alisema kwa hiyo wanapiga hatua kubwa kwenye kuhudumia shehena nyingi katika Bandari ya Tanga na kuhudumia shehena kwa ushoroba wa Kanda ya Kaskazini na wanafarajikia kwa mara ya kwanza kwa nchi ya DRC na Zambia mzigo mkubwa unaopita hapo ni Copper ambapo zaidi ya tani 30,000 zimehudumiwa hapo.
Alisema kwamba mteja wao huyo alikuwa akifanya huduma za kibandari katika Bandari ya Dar lakini kutokana ana uwekezaji uliofanywa na Serikali wa Bilioni 429 .1 kwa awamu zote mbili kuboresha bandari ya Tan