NA ASHRACK MIRAJI,LUSHOTO
MKUU wa wilaya ya Lushoto mkoani Tanga Japhari kubecha amesema maandalizi ya Tamasha la Utalii la Usambara yamekamilika.
Ameyasema hayo kkuelekea Tamasha la hilo ambalo linatarajiwa kufanyika Septemba 6 – 7 , 2024
Akizungumza na Mwandishi wetu ofisini kwake DC huyo amesema Wilaya ya Lushoto ni wilaya pekee ambayo imebarikiwa Kuwa na vivutioa vingi vya kitalii na ni wilaya ambayo imebarikiwa Kuwa na rasilimali nyingi ambazo wawekezaji wanaweza kuja kuwekeza na kufanya biashara zao za kiuchumi Kwa kushirikiana na serikali Katika kulijenga Taifa letu
Wilaya ya Lushoto imegawanyika katika Halmashauri mbili ambazo ni Lushoto na Bumbuli ukizingatia halmashauri ya bumbuli imebarikiwa ardhi yake kuwa na madini mbalimbali ikiwemo dhahabu madini ya ulanga na bouxite ambayo kwa wingi wake yanapatikana Lushoto ambapo wachimbaji wadogo wadogo wananufaika na rasilimali hizo kujipatia kipato na halmashauri kupata mapato.
“Nitumie fursa hii kwa Watanzania wote hivi karibu tunakwenda kufanya Tamasha kubwa la kihistoria ambalo tumelipa jina la Usambara Tourism Festival kuja kujionea fursa mbalimbali ambazo zinapatikana hapa na tutatembea kwa pamoja kujifunza vitu vingi vya kihistoria katika Wilaya yetu
“Sambamba na hayo wawekezaji wa ndani na wa nje mnakaribishwa kuja kuwekeza biashara zenu hapa Lushoto milango ipo wazi kuanzia ofisi ya Mkoa mpaka ya wilaya tutawapa ushirikiano wa kutosha hili kuendelea na shughuli za kiuchumi kaika wilaya yetu”alisema DC Kubecha “.
DC Kubecha ameendelea kusema lengo la kufanya Tamasha hili ni kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan hasa Katika sekta ya utalii yeye amekuwa kinara wa sekta hii tumeshuhudia mapato na Wageni wengi wanakuja Tanzania kutembelea Utalii wetu kufanya uwekezaji hapa nchini kupitia filamu yake Royal Tour.
Hivi karibuni wakati akizindua safari za treni ya mwendokasi inayotumia umeme SGR Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema safari za treni hiyo itakuwa ni kitovu Cha utalii hapa nchini na watalii watapata fursa ya kufika Mikumi kwa urahisi kabisa.
” ukweli Mhe Rais amekuwa kiongozi hodari na ni Mama mlezi hasa Kwa sisi vijana wake lazima tufanye kazi ili tuweze kumsaidia”
“alisema Kubecha”.