NA MWANDISHI WETU, DODOMA
WAZIRI wa Viwanda na Biashara Selemani Jafo ameelekeza Mita zote za Umeme kupelekwa kwa Wakala wa Vipimo(WMA) kwaajili ya kupimwa.
Lengo la kupima Mita hizo ni kutazama udhibiti wake ili kupunguza kulipa gharama zisizostahili kwa wananchi .
Jafo alitoa kauli hiyo Julai 17, 2024 jijini Dodoma alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Wakala huo, lililopo eneo la Medeli.
“Naelekeza mita zote za umeme na maji lazima zifikishwe Wakala wa Vipimo ili kuzipima kuangalia uthibiti wake kwa lengo la kuwapunguzia gharama wananchi. Isije mtu akafungiwa mita ambayo haina ubora, mwisho wa siku akalipa bili isiyo stahili,” alisisitiza.
Naye Mwakilishi wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa WMA, Joseph Maliti alitoa ahadi kwa Waziri kuwa WMA itahakikisha maelekezo yake yote yanatekelezwa.