NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
TANGU siku ya kwanza nakanyaga kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 48 maarufu kama Sabasaba nilivutiwa na banda la Shirika la Bima la Taifa NIC Insurance.
Nakumbuka ilikuwa Juni 30,2024 ikiwa ni siku mbili tu tangu maonesho kuanza yaani Juni 28,2024.
Kila nilipopata nafasi ya kuingia kwenye banda la NIC Insurance nilikuwa sikosi kitu kipya cha kujifunza hadi maonesho yalipohitimishwa rasmi jana Julai 13,2024 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi.
Mvuto ulikuja kutokana na mpangilio uliopo ndani ya banda la NIC,Usafi, ukimya,utulivu ,huduma zinazotolewa sambamba na unadhifu wa watoa huduma uliokuwapo.
Watoa huduma wake walikuwa ni watu walio na nyuso za tabasamu muda wote si asubuhi sio jioni mida ya lala salama.
Pia watoa huduma wote walikuwa na utayari kutoa elimu kwa kila anayeingia bandani kwao hata kwa mambo ambayo mtu hakuyaukiza basi wao wakitengeneza mazingira ya kumfanya mtembeleaji atoke akiwa na ufahamu na maarifa zaidi juu ya Bima.
Kama hiyo haitoshi uwe mteja usiwe mteja utahudumiwa vizuri katika kila eneo.
Binafsi ni miongoni mwa waliobahatika kutembelea banda hilo ambalo kwa utoaji huduma ule ni dhahiri shahiri NIC haikupewa ushindi wa kubebwa…wanastahili,walistahili ushindi kwenye Sekta ya Bima.
Ikumbukwe kwamba mbali ya Bima zingine,mwaka huu katika msimu wa Sabasaba ilijikita zaidi kuzitangaza Bima za Comesa,Majaliwa na Huduma ya Nisogeze .
Kimsingi elimu juu ya Bima na huduma hizo mpya zilibeba maudhui yenye mvuto yenye kumshawishi mtu yeyote yule kujiunga ili kupata fidia stahiki pindi yanapotokea majanga.
Nikirejea miaka kumi ya nyuma,NIC Insurance halikuwa Shirika zuri kusikika masikioni mwa watu kwasababu halikuwa likifanya vizuri ikilinganishwa na miaka mitatu ya hivi karibuni.
NIC Insurance ilikuwa ikionekana ni Taasisi iliyozeeka lakini hivi sasa mambo yamebadilika NIC imehuishwa na kuwa ya vijana.
Kwa mantiki hiyo imeifanya kuitendea haki kauli mbiu yao ya ‘Sisi Ndiyo Bima’ ambayo kutokana uwajibikaji leo hii NIC imeweza kuwa kinara katika utoaji huduma bora kiasi cha kupata Tuzo ya Super Brands Afrika Mashariki.
Bado naona mambo mengi mazuri kutoka NIC Insurance siku za usoni kwaajili ya Watanzania kwani ni Shirika ambalo lina wataalamu na litaendelea kuwa nao wa kutosha kwa mustakabali wa maendeleo ya Sekta ya Bima na Taifa kwa ujumla.
Niishauri NIC Insurance kutobweteka , iendelee kufanya kazi kwa juhudi na kuhamasisha umuhimu wa Bima kwetu sisi Watanzania .
Pia ifanyie kazi mapungufu madogo madogo ya huduma yaliyopo ili kuondoa malalamko ya wateja na kuendelea kuling’arisha zaidi Shirika .
Mwisho kabisa nihitimishe kwa kuipongeze NIC Insurance wa utendaji kazi wake hasa kwa waliopita na waliopo hivi sasa kwani kila mmoja ana mchango wake katika utendaji wake na mafanikio ya Shirika.