NA MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAM
KITUO cha Mikutano APC Hotel and Conference Centre kimepongezwa kwa kuendelea kutoa elimu na huduma kwa jamii pamoja na kuzalisha ajira mbalimbali kwa vijana Nchini.
Hayo yamebainishwa leo Julai 06,2024 na Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA. Prof. Sylvia S.Temu wakati alipotembelea banda la Kituo hicho katika Maonysho ya sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. Julius Nyerere
Amesema Kituo hicho cha APC kimekuwa kikitoa huduma mbalimbali ikiwemo huduma za hoteli, kumbi za mikutano zenye uwezo wa kubeba watu wengi.
Aidha CPA Prof. Temu amesema kuwa kituo hicho kimekuwa kikitoa Fursa za ajira kwa vijana na kuwataka watanzania kuendelea kuchangiamkia fursa mbalimbali zinazojitokeza ili kuweza kujikwamua kiuchumi
Katika hatua nyingine CPA Prof. Temu ametumia fursa hiyo kuwataka Watanzania kutembelea banda hilo ilikujionea jinsi ambavyo Kituo hicho kimekuwa kikiendelea kuvutia wawekezaji kupitia huduma mbalimbali.