ASHRACK MIRAJI,SAME
MBUNGE wa Jimbo la Same Magharib Dk. David Mathayo amewataka vijana wilayani humo kutumia fulsa ya michezo kuendeleza ushirikiano Kwa ajili ya shughuli za uzalishaji wa pamoja Ili kuleta Maendeleo katika wilaya hiyo
David Mathayo ameyasema hayo leo Juni 23,2924 Wakati wa uzinduzi wa msimu wa pili wa Mashindano ya Mathayo Cup 2024 yaliyofanyika katika viwanja vya Ruvu Jimbo la Same Magharibi wilayani hapa ambapo timu hizo zitatimua vumbi mwaka huu kwenye Mashindano hayo na zaidi ya timu 75 zitashiriki Mashindano ya mpira wa Miguu.
Amesema Msimu wa Mwaka Jana Wakati wa uzinduzi wa Mathayo Cup timu ambazo zilijitokeza 53 ukilinganisha na msimu wa pili, inaonesha vijana wanavyoamasika kwenye michezo timu hizo zitachuana kwenye Jimbo la same Magharib hivyo mshindi wa kwanza katika Mashindano hayo atakabidhiwa kitita ,cha sh Sh.7,000,000 na Mshindi wa pili atakabidhiwa Sh .5,00,000 na Mshindi wa tatu atakabidhiwa Sh.3,500,000 3 na wanne atakabidhiwa Sh.1,000,000
Sambamba na hayo yote Dk.Mathayo Aliendelea kusema Mashindano hayo yanatumika kuwahamasisha vijana kujitokeza Kwa wingi kushiriki kikamilifu uchaguzi wa serikali za Mitaa pia yanatumika kueleza kazi ambazo zimefanywa na serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan pamoja na kuwakumbusha Miradi Mbalimbali ya Maendeleo inayotekelezwa wilaya ya Same hasa katika jimbo la same Magharib, Ili watakapofanya uchaguzi wafanye uchaguzi Sahihi.
Katibu Mwenezi wa wilaya ya Same Mohamed Ifanda Ambaye ni Mgeni Rasmi kwenye Mashindano hayo amesema kuwa anampongeza Mbunge wa Jimbo Hilo David Mathayo Kwani kwa sasa Jimbo la Same Magharibi linaelezea utekelezaji wa ilani ya Chama Cha mapinduzi inayotekelezwa Katika nchi hii vijana wanapokuwa wanaitwa pamoja na wanafanya michezo kwani hawafikirii mambo mengine bali ni michezo tu hii inawajengea mahusiano mazuri baina ya wao wenyewe na serikali
“Niwaombe vijana mnaoshiriki Mashindano haya kuwa wanzalendo wa Taifa letu na wilaya Kwa ujumla pia Kuacha Mambo yasiyo mazuri kama uvutaji bangi uuzaji mirungi ukabaji tumieni michezo hili kubadili taswira ya Taifa letu michezo ni ajira michezo inaleta fursa mbalimbali za Maendeleo hapa nchini tumieni muda mwingi katika kujishuhulisha kwenye michezo hii ambayo imeanzishwa na Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi Mathayo kwa lengo la kuwataka vijana wawe na fikra chanya katika nchi yao na kushirikiana kwa pamoja katika kuleta Maendeleo” amesema Ifanda
Dk. Mathayo ameamua kuonesha vijana wa Jimbo la Same Magharib wana nguvu ya kucheza mpira kazi anayoifanya ni kubwa kupitia vijana hawa maana unaposema timu 75 wapo vijana Zaidi ya 2000 hili siyo jambo dogo ni jambo kubwa la kuigwa katika Mkoa wa Kilimanjaro
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Mathayo Cup Raphael Senkoro amesema michezo katika Jimbo Hilo inaweza kukuza vipaji vya vijana wa Same na kwamba michezo ni Afya, Ajira.
Senkoro amempongeza Dk.Mathayo kwa kutambua kundi hioi la vijana hasa wanaoshiriki michezo hiyo kwenye maeneo yetu na kuwaomba Madiwani wawe wanafanya Kijiji kwa Kijiji ikiwezekana itakapofika kipindi cha Mathayo Cup kila Kata ije imejipanga kwa ubingwa