NA MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAM
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano w Tanzania Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika uzinduzi rasmi wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura utakaofanyika Julai Mosi mwaka huu mkoani Kigoma.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ( INEC Jaji Jacobs Mwambegele mapema leo asubuhi Juni 13,2024 katika ufunguzi wa Mkutano baina ya INEC na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam.
” Uboreshaji wa taarifa za Mpiga Kura utajumuisha wale wote wenye sifa za kupiga kura ambapo INEC itatoa kupaumbele kwa wenye Ulemavu ,Wazee na akina mama wenye watoto.
“Tume inayataka makundi tajwa kujitokeza kwa wingi katika uboreshaji huo wa taarifa za Mpiga Kura katika Daftari hilo la Kudumu ” amesisitiza Jaji Mwambegele
Pamoja na mambo mengine Jaji Mwambegele ameeleza juu ya elimu inayoendelea kutolewa kwa wananchi ili kuwa na uelewa juu ya zoezi hilo ambapo INEC imeahidi kuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa.