NA MWANDISHI WETU, MOROGORO
WAHITIMU wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kilichopo mkoani hapa wameaswa kutumia elimu na mafunzo waliyopata chuoni hapo kwa ubunifu katika kufanya maendeleo endelevu kwa ustawi wa taifa la Tanzania.
Kauli hiyo imetolewa Mei 23,2024 na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman wakati akitoa hotuba kwenye Mahafali ya 43 ya katikati ya mwaka ya Chuo yaliyofanyika kwenye Kampasi ya Edward Moringe, Morogoro ambapo zaidi ya wanafunzi 700 walihitimisha safari ya masomo yao.
Alisema kwa niaba ya Baraza la Chuo wanakusudia kuona ubunifu kwa wahitimu kwenye shughuli ambazo watakuwa wanafanya ili kuleta teja katika maisha yao kiuchumi, taaluma na manufaa kwa taifa kwa ujumla.
“Mnapoingia kwenye ulimwengu wa ajira iwe ya kuajiriwa au ya kujiajiri kumbukeni kuwa ninyi ni Mabalozi wetu katika kutunza maadili , ubunifu, na uchapakazi
“Maarifa na ujuzi mlioupata hapa ziwe dhana za kuleta mabadiliko chanya kushughulika na matatizo ya nchi na za kidunia na kuboresha maisha ya watanzania na jamii kwa ujumla,” alisisitiza Jaji Mkuu Mstaafu Chande