NA MWANDISHI WETU, DODOMA
NAIBU Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geofrey Mizengo Pinda amesema Wizara yake ipo tayari kutoa ushirikiano kwa Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Wizara za Kisekta kuweka mipango ya matumizi bora ya ardhi ikiwa ni hatua muhimu ya kukabiliana na migogoro ya Ardhi inayotokana na jamii za vijijini kuvamia maeneo ya Taasisi hizo.
Naibu Waziri Pinda amesema hayo mapema juzi wakati wa hotuba ya ufunguziwa Kikao cha Wadau na Tume ya Taifa ya Matumizi ya ardhi alipomwakilisha Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa kufungua Mkutano huo jijini Dodoma.
Aidha ameitaka Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi kushirikiana na Wizara ya Mali Asili na Utalii kuchukua hatua za haraka na mapema ili baadae isije kulazimika kutumia nguvu kuondoa watu katika eneo la ushoroba wa wanayama hao.
Katika hatua nyingine Waziri Pinda amezitaka mamlaka za upangaji nchini ambazo ni Halmashauri zote nchini kuhakikisha mipango yote iliyoandaliwa kwa kushirikiana na wadau inawasilishwa Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi ili ziweze kusajiliwa ili ziweze kupatiwa na kutangazwa katika Gazeti la Serikali.
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga amewambia wajumbe wa Kikao Kazi hicho kuwa Idadi ya Watu katika Vijiji imekuwa kiongezeka kwa watani wa asilimia 2.4 kwa mwaka akibainisha kuwa vijijini kuna kaya zaidi ya Mil.8.6 sawa na asilimia 60.3 ya Kaya zote Nchini.
Katika hatua nyingine Waziri Pinda amezitaka Mamlaka za upangaji nchini ambazizo ni Halmashauri zote nchini kuhakikisha mipango yote iliyoandaliwa kwa kushirikiana na wadau inawasilishwa Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi ili ziweze kusajiliwa ili kupatiwa na kutangazwa katika Gazeti la Serikali.
Kufuatia hali hiyo Mhandisi Sanga alisema Ardhi hiyo ikipangwa, kupimwa na kumilikishwa itakuwa inachangia maendeleo ya kiuchumi ikiwemo usalama wa chakula na mtaji muhimu katika kuondoa umasikini hapa Nchini.
Wakati huo huo Mkurugenzi wa Tume ya Matumizi Bora ya Ardhi Prof. Wakuru Magigi alibainisha kuwa ifikapo Juni mwaka huu Mipango yote ya Upangaji Vijiji Nchini itakuwa jumla ya Mipango