*WASEMA WANATAKA NISHATI YA UHAKIKA
[Uchambuzi wa ACT Wazalendo kuhusu Bajeti ya Wizara ya Nishati kwa Mwaka wa Fedha 2024/25]
Utangulizi
Mei 23, 2024 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipokea na kuanza kujadili hotuba ya bajeti Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2023/24 kutoka kwa Waziri wa Nishati na Naibu Wazii Mkuu Dr. Doto Mashaka Biteko (Mb). Wote tunafahamu kuwa bajeti ni nyenzo muhimu sana katika utekelezaji wa miradi na programu, uhakika wa upatikanaji na ugharamiaji wa huduma ya nishati.
Katika mwaka huu wa fedha 2024/25 Wizara ya Nishati imeomba kuidhinishiwa kiasi cha shilingi trilioni
1.88. Ambapo shilingi trilioni 1.79 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo sawa na 95.3% na kiasi kilichobaki cha shilingi bilioni 88.9 kwa matumizi ya kawaida. Ikilinganishwa na mwaka wa fedha uliopita kiasi bajeti ya mwaka huu imepungua kwa shilingi trilioni 1.2 sawa na asilimia 38.1. Aidha, tumeshuhudia kushuka kwa 3.01% wa uwiano wa bajeti ya wizara ikilinganishwa na bajeti kuu ya Serikali mwaka 2024/25 shilingi trilioni 49.34 ni sawa na 3.8%.
Katika uchambuzi wetu wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/25 tumekuja na maeneo nane (8) yenye changamoto na tumeyatolea maoni ili kuhakikisha bajeti ya mwaka huu inayazingatia kwa ajili ya kuimarisha upatikanaji wa nishati nchini.
Katika hoja hizi tumeangazia; uhakika wa upatikanaji wa huduma ya umeme, mafuta na gesi (nishati); Gharama za kupata huduma hizo; vipaumbele vinavyowekwa na Serikali kwenye kushughulikia changamoto, uanzishaji na utekelezaji wa Miradi; usimamizi wa matumizi ya fedha zinazoelekezwa kwenye miradi ya maendeleo na kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo.
- Hali ya upatikanaji wa huduma ya umeme nchini.
Katika zama tulizonazo hali ya upatikanaji wa huduma ya umeme ya uhakika huchochea ukuaji wa uchumi (Uzalishaji viwandani na mashambani) na utoaji wa huduma zingine kama vile elimu, mawasiliano, usafiri na uchukuzi, matibabu na huduma za utawala. Kwa hiyo, umeme una nafasi na mchango mkubwa sana katika maisha yetu kama jamii na nchi kwa ujumla wake.
Pamoja na umuhimu huu tunaona huduma ya umeme nchini bado sio ya uhakika kumekuwa na changamoto ya muda mrefu ya kukatika kwa umeme mara kwa mara. Kwa hali hii ni wazi kuwa kutosimamiwa vyema huduma ya upatikanaji wa umeme unarudisha nyuma uwekezaji mkubwa kwenye viwanda, mitaji na maisha ya watu, kuzoretesha mifumo mingine ya huduma kama vile matibabu, uchukuzi na mawasiliano na masuala ya utawala.
Mwenendo wa uwezo wetu wa kuzalisha umeme kwa mujibu wa taarifa za wizara kutoka kwenye hotuba ni kuwa uzalishaji wa umeme nchini kwa mwaka hadi March 2024 ni megawati 2,138 ni sawa ongezeko la asilimia 14.2 mahitaji ya juu ya umeme katika mfumo wa Gridi ya Taifa yameongezeka na kufikia MW 1,590.1 ikilinganiswa na mwaka jana Ambapo yalikua MW 1,470.5 sawa na ongezeko la asilimia 8.1
Kwa upande wa ongezeka la mahitaji kutokana na usambazaji wa umeme vijijini linakuwa kwa asilimia 17.8. Ni dhahiri kuwa kasi ya uzalishaji na usambazaji wa umeme haulingani, jambo linalopelekea kuwa na upungufu wa uwezo wa kuhudumia wananchi. Ndio maana tunashuhudia kukatika kwa umeme mara kwa mara. Aidha, miradi mingi ya usambazaji bado inasuasua na mpaka sasa Vijiji mia nne themanini na moja (481) havijaunganishwa na umeme nchini.
ACT Wazalendo, tunaitaka serikali kuacha hadaa kwa wananchi kuwa tatizo la upatikanaji wa Umeme limekwisha nchini badala yake waweke nguvu katika usambazaji wa Umeme haraka ili wananchi waweze kujiendeleza kiuchumi, ni wajibu wa serikali kuhakikisha nchi ina nshati ya kutosha.
- Utitiri wa miradi ya umeme na ufinyu wa upatikanaji wa fedha za utekelezaji.
Mwaka wa fedha 2023/24 tulionyesha namna Serikali inavyotawanya nguvu kiduchu ya fedha iliyopo kwenye miradi mingi ya kuzalisha na kusafirisha umeme. Kwa zaidi ya miaka minane imekuwa ikitajwa kama miradi ya kipaumbele bila kukamilika na huku ikitengewa fedha kiduchu za utekelezaji wake au mingine kutotengewa kabisa. Tulitahadharisha mwenendo huu wa uwekaji vipaumbele na usimamizi wa utekelezaji wake kwa kuonyesha mchanganuo wa miradi 10 ya uzalishaji na usafirishaji wa umeme iliyotawanywa nchi nzima bila kukamilika kwa miaka mitano (5).
Aidha, tulionyesha mwenendo na hali ya upatikanaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo kwa miaka miwili mfululizo. Kwa mwaka wa fedha 2020/2021 wizara ilipanga kutumia Sh. trilioni. 2.197 lakini hadi kufikia Aprili 2021 ilipokea ShT. trilioni 1.35 sawa na asilimia 61.5 ya bajeti yote. Kwa mwaka 2021/22 wizara ilipanga kutumia shilingi trilioni 2.386 hata hivyo ilipewa shilingi Trilioni 1.820 sawa na asilimia 76.29 ya bajeti yote katika kipindi kama hicho katika bajeti ya mwaka jana 2023/2024 wizara iliidhinishiwa na Bunge Shilingi Trilioni 3.04 lakini mpaka kufikia mwezi mwachi 2024 ni Trilioni 1.8 pekee ndio zimepokelewa sawa na asilimia 59.4 ni wazi kwa kipindi kilichobakia kufikia mwezi Juni, bajeti hiyo haitotolewa kwa ukamilifu wake.
Katika mwaka mwa fedha 2024/25 tumeona Serikali ikiendelea na utaratibu ule ule wa kuorodhesha utitiri wa miradi na kutawanya fedha bila kukamilisha malengo ya kuzalisha umeme ambao ungeweza kuendana na kasi kubwa ya ukuuaji wa mahitaji ya umeme. Kutokana na utitiri wa miradi tumeona kwa mwaka 2023/24 Serikali imeweza kukamilisha Mradi wa Rusumo ambao umechukua miaka 8 tangu 2015. Huku ongezeko la uzalishaji wa umeme kwa mwaka huu umekuwa Megawati 251 kutoka Bwawa la Mwl. Nyerere na Rusumo kwa MW 235 na 26MW mtawalia.
Orodha ya baadhi ya miradi ya kipaumbe iliyopo kwenye hatua ya utekelezaji na kutengewa fedha kwa mwaka huu ni kama ilivyo hapo chini;
- Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Julius Nyerere (JNHPP) – MW 2,115 Shilingi bilioni 620
- Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Rusumo – MW 80
- Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Malagarasi – MW 49.5
- Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Jua Mkoani Shinyanga – MW 150
- Miradi ya Kuboresha Upatikanaji wa Umeme Mikoa ya Kusini (Lindi na Mtwara)
- Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Gesi Asilia wa Kinyerezi I Extension MW 185
- Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Kikonge – MW 321
- Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Kakono MW 87.8
- Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Ruhudji MW 358
- Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Rumakali MW 222
- Ukarabati wa Kituo cha Kufua Umeme cha Hale Hydro Power Plant
- Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Malagarasi MW 49.5
Kwa upande wa miradi ya usafirishaji na usambazaji wa umeme nayo ipo miradi zaidi ya 15 baadhi ya miradi hiyo kama inavyoonekana hapa chini.
- Julius Nyerere Hydro Power Plant hadi Chalinze-kV 400 na Kituo cha Kupoza Umeme, Chalinze
- Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa kV 220 kutoka Geita hadi Nyakanazi na Kituo cha Kupoza Umeme, Nyakanazi
- Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa kV 400 kutoka Singida-Arusha-Namanga na Kituo cha Kupoza Umeme, Lemugur
- Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa kV 400 kutoka Nyakanazi hadi Kigoma na Kituo cha Kupoza Umeme, Kidahwe
- Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa Kilovoti 400 kutoka Iringa hadi Sumbawanga kupitia Mbeya na Tunduma (TAZA)
Wakati wizara inaianzisha miradi hii ilijiwekea malengo ya kukamilika ifikapo mwaka 2025. Kwa mwenendo huu wa bajeti ambapo mpaka sasa wizara haijapata hata asilimia 30 ya fedha inazozihitaji kukamilisha miradi hii, ndoto ya kuzalisha MW 5000 za umeme ifikapo 2025 haziwezi kufikiwa huku baadhi ya miradi ikikumbwa na harufu za rushwa na uzembe unaoligharimu taifa kama tutakavyoainisha.
ACT Wazalendo tuna maoni kuwa Serikali ijikite kwenye miradi michache itakayotoa matokeo kwa kuzingatia uwekezaji ambao tumeshaufanya na ijikite kwenye uwezekano wa nchi kujitosheleza kwa nishati ya umeme kabla ya kufikiria kuuza umeme nje ya nchi. Kwa kufanya hivi tutaokoa fedha nyingi zinazolipwa kama riba ya kuchelewa kutekeleza mikataba kwa wakati na kuziba mianya ya wizi kwa utitiri wa miradi isiyojulikana itakamilika lini.
- Utekelezaji wa Miradi ya Bwawa la Kufua umeme la Julius Nyerere na Mradi wa kusindika Gesi Asilia Lindi (LNG)
Nchi yetu ipo kwenye mpango wa kuhakikisha inakuwa na nishati ya uhakika na ghrama nafuu. Hivyo, imekuwa ikiitaja miradi mikubwa miwili kama ndio injini ya kutufikisha kwenye ndoto ya kuwa na uhakika wa uzalishaji wa umeme. Changamoto kuwa za jumla katika miradi hii ni kuchelewa kutekelezwa kwake. Ndio hoja ya muda mrefu tuliyokuwa tunairudia rudia katika mapendekezo yetu. Lakini, kwa hatua kadhaa kila Mradi unachangamoto Mahususi kama tunavyozifafanua hapa chini.
- Mradi wa kusindika Gesi Asilia wa Likong’o, Lindi.
Katika hotuba ya bajeti Waziri amelieleza bunge kukamilika kwa mazungumzo na Wawekezaji, ya Mkataba wa Nchi Hodhi (Host Government Agreement-HGA) na Mkataba wa Uzalishaji na Ugawanywaji Mapato (PSA), kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia kuwa Kimiminika (Liquefied Natural Gas – LNG) lakini mpaka sasa Serikali bado inaburuza miguu.
Wakati tunaenda kwenye uwekezaji huu wa mradi mkubwa kuna changamoto ya kuwa na maandalizi madogo ya kuwawezesha wenyeji kushiriki na kufaidika na uwekezaji huu; malalamiko ya wananchi waliohamishwa kwenye ardhi zao kucheleweshewa na kupunjwa kwa fidia; pia, mfumo mbovu wa sera ya fidia ya ardhi kwenye maeneo ya miradi.
Pia, suala la maandalizi tunaona bado mji wa Lindi haujaandaliwa, vyuo vya ufundi stadi (VETA) kwa miaka yote havijafungamanishwa kuandaa mafundi, wataalamu na wasaidizi kuupokea Mradi huu.
Waziri ameliambia Bunge kuwa Serikali kupitia TPDC imeendelea kushirikiana na Kampuni za Shell na Equinor kufanya maandalizi ya kutekeleza miradi ya uboreshaji wa hali ya maisha kwa wananchi waliopisha eneo la mradi (post compensation livelihood restoration program), ambapo mpaka sasa lililofanyika ni kusaini Mkataba wa Makubaliano ya ujenzi wa shule ya msingi ya Likong’o iliyopo Manispaa ya Lindi. Hii ni kasi na kiwango kidogo sana ukilinganisha na thamani ya Mradi huo.
ACT Wazalendo inatoa wito kwa Serikali kufanya haraka na kwa uwazi utekelezaji wa mradi huu wa kielelezo kwa nchi yetu.
Pili, katika mazungumzo yanayoendelea kati ya TPDC, Serikali na Wawekezaji wa Mradi wa LNG ni muhimu suala la Manispaa ya Lindi kumiliki angalau 2.5% ya Mradi mzima lizingatiwe na mchango wa manispaa uwe ni Ardhi yake kama Mtaji (land for equity).
- Mradi wa Bwawa la kufua Umeme la Julius Nyerere- Rufiji
Mradi ulianza mwaka 2019 na ulitarajiwa kukamilika mwezi Juni mwaka 2022. Mradi huu wenye thamani ya shilingi trilioni 6.55 bado haujakamilika mwaka jana walisema utakamilika Juni, 2024. Katika bajeti ya mwaka huu, Serikali inasema Mradi huu utakamilika ifikapo Desemba, 2024.
Ucheleweshwaji wa Mradi wa JNHPP unaendelea kuligharimu taifa kwa kulipa fedha za ziada kwa wakandarasi, kuendelea kutokuwa na uhakika wa umeme na atahri zingine za kijamii kama vile mafuriko na kutotolewa kwa fedha miradi kwa jamii.
Hadi kufikia mwaka huu gharama za ziada kwa mujibu wa ripoti ya CAG ya mwaka 2021/22 ni shilingi bilioni 327 nyongeza anayopaswa kulipwa mkandarasi. Pia, kuna ucheleweshwaji wa manunuzi ya vifaa vya umeme na mitambo ndio maana hadi leo kati ya mitambo 9 inayopaswa kuzalishia umeme ni mtambo mmoja pekee umekamilika na kuwasha. Waziri anasema watawasha mwingine hivi, karibu. Karibu sijui ni lini.
Ukiachilia, gharama tunayolipa kama taifa kutokana na ucheleweshwa huu. Tumeona katika siku za hivi karibuni kuongezeka zaidi kwa changamoto juu ya uhakika wa upatikanaji wa umeme nchini. Katika mazingira ambayo bwawa limepokea maji ya kutosha (limejaa) lakini kinu cha kuzalisha umeme kilichofunguliwa ni kimoja (1) kati mitambo 9. Kwahiyo umeme unaozalisha ni Megawati 235 pekee kati ya Megawati 2115 zilizotarajiwa.
Tunashangaa kuona Wizara ya Nishati kupitia TANESCO imefungulia maji ambayo yameenda kusababisha maafa makubwa kwa wakazi wa Rufiji na Kibiti. Badala ya kutumia maji hayo kuzalishia umeme wa kutosha. Hivyo basi, ucheleweshaji na uzembe mkubwa katika usimamizi wa Mradi huu umeligharimu taifa letu sio tu fedha zilizoteketea kwa kulipa ziada bali maisha ya watu kutokana na mafuriko.
ACT Wazalendo tunamtaka Waziri wa Nishati ambae pia ni Naibu Waziri mkuu kuhakikisha fedha za Wajibu kwa jamii (CSR) zinatolewa na kufanywa miradi husika kwa wakati ili zisaidie kuiendeleza Rufiji na wakazi wake.
- Matumizi ya nishati Safi kwa ajili ya kupika
Tayari Serikali imeidhinisha mkakati wa nishati Safi ya Kupikia mwaka 2024-2034. Nishati safi ya kupikia ni rafiki wa mazingira na afya ya mwanaadamu inakadiriwa kwamba kila mwaka hekari milioni moja ya miti inakatwa kwa matumizi ya kuni na mkaa. Tayari matamko yametolewa yakisisitiza taasisi za umma na binafsi kusitisha matumizi ya kuni na mkaa ifikapo Januari 31 mwaka 2025.
Mjadala huu unaibuwa uhitaji mkubwa wa nishati mbadala utakaobadilisha utamaduni wa matumizi ya kuni na mkaa uliopo nchini. Tafiti zinaonesha Asilimia 92 watanzania hawatumii nishati safi ya kupikia, hii ni kutokana na sababu kadhaa za upatikanaji wa Nishati safi ya Kupikia, mfano Gesi kiwango cha chini ni shilingi 24,000.
Serikali ya CCM kwa kiwango kikubwa inawekeza kwenye makongamano na kusifia badala ya kuweka nguvu kuhakikisha upatikanaji wa nishati safi nchini, wakati asilimia 92 ya watanzania hawatumii nishati safi tayari Serikali ya CCM imeanza mpango wa kuuza Gesi nchini Kenya ambapo mradi wa Kusafirisha Gesi asilia kutoka Dar es salaam hadi Mombasa (Kenya) na waziri ameliambia Bunge kuwa kamati za wataalamu zimesha kamilisha baadhi ya taratibu
Wakati Serikali ya CCM inajiandaa kupeleka Gesi nchini kenyua CAG anasema kuna Ucheleweshaji wa kuanza na kukamilika kwa miradi ya usambazaji wa gesi asilia kwa matumizi ya nyumbani shilingi bilioni 17.23 kwa miradi ya barabara ya bagamoyo, chuo kikuu Dar es salaam na Mkurangaambapo miradi hiyo ilipaswa kukamilika kufikia tarehe 30 Juni 2023, hata hivyo miradi hiyo ilikuwa katika hatua za awali. CAG anasema Utekelezaji ulicheleweshwa kutokana na kutotolewa kwa fedha za kutosha kutoka kwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kuchelewa kuidhinishwa kwa vibali kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), mchakato wa ununuzi usio na ufanisi, na kuchelewesha malipo ya awali kwa makandarasi lakini serikali ya CCM inakimbilia kuuza gesi nje ya Nchi huku wananchi wakiendelea na matumizi ya Kuni na mkaa.
ACT Wazalendo tunaitaka serikali kuwekeza kuhakikisha Watanzania wananufaika na utajiri wa gesi, serikali ya CCM iweke kipaumbele wananchi wan chi hii na sio maslahi ya wafanyabishara wachache, tatizo la Nishati safi nchini halitamalizwa na makongamano na mabango bali kazi ya usambazaji wa gesi kwa wananchi kama ambavyo serikali iliahidi.
- Usimamizi wa uingizaji wa Mafuta nchini.
Kwa miaka mitatu ya bajeti kuanzia 2021 hadi 2024 pamekuwepo na tatizo la kupanda kwa gharama za mafuta ya Nishati (Petroli, Diseli na mafuta ya taa). Vile vile, robo ya pili ya mwaka fedha unaoishia Juni, 2024 tuliona kuongezeka kwa changamoto ya upatikanaji wa mafuta (uhaba wa mafuta). Tatizo la upatikanaji wa mafuta na gharama zake linahitaji hatua za makusudi za Serikali kuliko kusubiri sababu za nje.
Mwaka 2022/23 Mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali (CAG) amefanya ukaguzi wa Ufanisi kwenye eneo la usimamizi wa uagizaji wa mafuta nchini. CAG ameonesha kuwa nchi yetu haina hifadhi ya kimkakati ya mafuta ya Petroli kiasi cha kutishia usalama wa nchi. Aidha, CAG ameonyesha kuanzia mwaka 2020 hadi 2023 zinaonesha kuwa kampuni za uangizaji wa mafuta hazikuhifadhi mafuta ya kuweza kutumika kwa siku 15 wakati wote kati ya asilimia 12 hadi 62, na asilimia 14 hadi 65 kwa petroli na dizeli mtawalia.
Hii ni kutokana na Uzembe wa EWURA kufuatilia na kutathimini uwezo wa kampuni hizo badala yake ilikuwa inafanya makadirio ya jumla tu. Hivyo kupunguza uwezo wa kutambua kampuni ambazo hazikuhifadhi mafuta yanayotakiwa. Vilevile, CAG ameonyesha kukosekana kwa ripoti ya ukubwa wa soko kwa kila kampuni na kwa kila bidhaa kulipunguza uwezo wake wa kubaini hatari kwenye uhakika wa ugavi wa mafuta.
Jambo, jingine lililoonyeshwa na CAG ni uwezo mdogo wa Miundombinu wa usambazaji wa mafuta. Anasema kwamba bomba moja tu linalotumika kuingiza mafuta Tanga, mtwara na Dar es salaam na Bomba hilo moja ndio hutumika kusafirisha Petroli na Dizeli. Kiasi baada ya kusafirisha petrol linasafishwa ili kupitishwa Dizeli hii imepelekea uchelewaji wa kupakua mafuta kutoka 66-68 na kuongeza gharama za uchelewaji kwa Dola za Kimarekani Milioni 26.93.
Ni wazi kuwa matokeo haya ya ukaguzi na hoja zingine zipelekea kupandisha bei zaidi na kuongeza kiwango cha uhaba zaidi nchini. Waziri mwenyewe anakiri kuwa mafuta katika soko la dunia yameshuka kwa wastani asilimia 7 wakati bei zilizotolewa na EWURA zikionyesha kupanda zaidi. Hata nchini Jirani Kenya na Uganda mafuta yameonekana kushuka.
ACT Wazalendo tunataka Serikali ijenge uwezo wa Miundombinu ya kisasa na usimamizi wa hifadhi ya Mafuta nchini, tuwe na angalau hifadhi ya mafuta kutumika kwa miezi mitatu ili kupanda kwa haraka kwa bei ya mafuta katika Soko la Dunia kusitutetereshe kwa haraka.
Pili, Serikali iboreshe Miundombinu ya kupokeana kusambazia Mafmuta nchini ikiwemo bomba la kisasa la mafuta.
Tatu, Serikali irejeshe ruzuku kwenye mfuta ya petroli na Diseli kwakuwa sababu zilizosababisha kuwekwa hazijaondoka
Aidha, ni wakati sasa Serikali kuweka msisitizo wa kupunguza matumizi ya mafuta ya Petroli na Diseli kwa kutumia nishati mbadala ya Gesi asilia. Hii inawezekana kwa kuchukua hatua kadhaa za haraka;
- Magari yote ya Serikali yaanze kutumia Gesi asilia (CNG) na bohari zote za Serikali (GPSA) zifungwe mitambo ya kujazia gesi asilia (CNG)
- Vilevile, mabasi ya mwendokasi nayo yabadilishwe mfumo na yaanze kutumia gesi asilia
- Pia, magari ya abiria ya mikoani (mabasi) yote yafungwe mfumo wa kutumia mitungi ya Gesi asilia (CNG), ili kupunguza kutumia fedha nyingi za kigeni kuagiza bidhaa za mafuta.
- Kasi ndogo ya Matumizi ya Gesi Asilia (CNG) nchini.
Changamoto ya upatikanaji wa mafuta na athari za matumizi yake ilipaswa kutumika kama sababu msukumo kwa Serikali kuongeza kasi katika kuhakikka taifa letu kutumika Nishati mbadala ambayo inapatikana nchini. Lakini tunaona kuna changamoto kuu mbili (2) kubwa; moja ni gharama kubwa za mfumo wa kutumia gesi na uhaba wa vituo vya kujazia gesi, licha ya hamasa kubwa waliopata watumiaji wa magari binafsi na waendesha bajaji kuhamia kwenye mfumo.
Katika bajeti ya wizara imeweka bajeti ndogo sana katika kuhakikisha taifa linahamia kwenye matumizi ya Gesi Asilia. Hotuba ya Waziri imeonyesha kwamba TPDC na GPSA ndio zipo kwenye hatua za awali za kufunga mifumo kwenye bohari za Serikali. Vile vile kuna karakana nane (8) za Serikali na binafsi zilizojengw kwa ajili ya kubadilisha mfumo wa magari kutumia gesi asilia. Karakana zipo Dar es Salaam pekee.
Hatua hizi zinaenda polepole sana ukilinganisha na uhitaji uliopo. Waziri ameliambia Bunge kuwa vituo vya kujazia gesi asilia ni vipo viwili tu kwa Mkoa mzima wa Dar es Salaam. Kituo kinachomilikiwa na kampuni ya Dangote kilichopo Mwanambaya Mkuranga na kituo cha kampuni ya TAQA-Dalbit kilichopo pembezoni mwa barabara ya Nyerere karibu na Kiwanja cha Ndege (Terminal II) hata hivyo tunazo taarifa kuwa kipo kituo kingine kidogo maeneo ya Vetenari.
ACT Wazalendo, hasa kwa kuzingatia mizozo inayoendelea katika nchi ya Israel na Iran na nchi za mashariki ya kati na vita Ukrain na Urusi, tunaitaka serikali
Mosi, Iweke msisitizo kwa TPDC na GPSA kufunga mifumo ya kuweka gesi kwenye gari za serikali haraka na gari zote za Serikali zifungwe mifumo hiyo.
Pili, serikali iweke mazingira wezeshi kwa wauzaji wa maguta wa rejareja kuwa na Pampu za gesi asilia (CNG) kwa ajili ya kutoa huduma zote na kuweka vivutio kwa wawekezaji wa ndani kuwekeza katika utoaji wa huduma hiyo.
Tatu, Tunawasihi wasafirishaji wa Mabasi na malori ya Mizigo kufunga mifumo ya Gesi asilia katika vyombo vyao.
Nne, Serikali kupitia Naib waziri Mkuu ambae pia ni waziri wa Nishati kwa kushirikiana na wazir wa Ujenzi kufanya tathmini ya gharama za ufungaji wa mifumo hiyo kwa vyombo vya usafiri kama gar ndogo na bajaji ili kuona namna ya kupunguza gharama ya kufungiwa mfumo huo.
Hitimisho.
Bajeti ni nyenzo muhimu sana katika kupima vipaumbele vya matumizi ya fedha za umma katika kukabiliana na changamoto za wananchi na upatikanaji wa huduma muhimu kwa wananchi. Katika kutazama bajeti ya mwaka huu ya wizara ya nishati trilioni 1.88 imepungua zaidi ikilinganishwa na mwaka uliopita. Hii inaweza kutoa picha kuwa bado haipewi kipaumbele sana kamwizara katika uwiano wa vipaumbele vya Serikali.
Ahsanteni sana.
Imetolewa na
Ndg. Philbert Macheyeki
Waziri Kivuli wa Nishati
ACT Wazalendo
April 24, 2024.
OFISI YA WASEMAJI WA KISEKTA.
TUNATAKA NISHATI YA UHAKIKA NCHINI.
[Uchambuzi wa ACT Wazalendo kuhusu Bajeti ya Wizara ya Nishati kwa Mwaka wa Fedha 2024/25]
Utangulizi
Jana Mei 23, 2024 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipokea na kuanza kujadili hotuba ya bajeti Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2023/24 kutoka kwa Waziri wa Nishati na Naibu Wazii Mkuu Dr. Doto Mashaka Biteko (Mb). Wote tunafahamu kuwa bajeti ni nyenzo muhimu sana katika utekelezaji wa miradi na programu, uhakika wa upatikanaji na ugharamiaji wa huduma ya nishati.