NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu ametangaza kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi
Rais Samia ametangaza kifo hicho wakati akilihutubia Taifa kupitia Vyombo mbalimbali vya Habari hivi punde.
Rais Dk Samia amesema Mzee Mwinyi amefikwa na umauti katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es salaam alipolazwa kwa matibabu ya Saratani ya Mapafu leo februari 29, 2024.
Taarifa zaidi zitakujia kadri tutakavyozipokea.