NA MWANDISHI WETU, PWANI
KAZI ya marekebisho ya Pampu ya kusukuma maji katika mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Chini imekamilika. Marekebisho haya yaliyosababisha upungufu wa uzalishaji maji kutoka lita Milioni 270 hadi lita Milioni 220 kwa siku.
Matengenezo yamekamilika februari 26, 2024 na kurudisha hali ya uzalishaji katika kawaida yake ya ujazo wa lita milioni 270 kwa siku.
Maeneo yafuatayo yataanza kupata huduma ya maji kwa msukumo mzuri
*Bagamoyo, Mapinga, Mabwepande, Bunju, Tegeta, Mbweni, Boko, Salasala, Goba, Mivumoni, Kawe, Lugalo, Makongo, Chuo, Kikuu, Mwenge, Kijitonyama, Mikocheni, Msasani, Oysterbay, Masaaki, Mwananyamala, Kinondoni, Magomeni, Kigogo, Chang’ombe, Keko, Kurasini, Kigamboni, Airport, Kiwalani, Buguruni, Vingunguti, Ilala na Katikati ya Jiji.