Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akizungumza na wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kutembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jana kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa. Kulia kwa Mhe. Waziri ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Dk.Faustine Ndugulile Mbunge wa Kigamboni na kushoto ni Naibu Waziri wa Afya Dk.Godwin Mollel.Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye pia ni misimamizi wa wodi ya watoto Theresia Marimo akiwaeleza wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi huduma za matibabu ya moyo wanazozipata watoto waliolazwa katika wodi hiyoMkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dk.Peter Kisenge akisoma taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi hiyo kwa wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kutembelea JKCI jana kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa.Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Deogratis Nkya akiwaonesha wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi jinsi wanavyofanya upasuaji wa kuzibua tundu la moyo wa mtoto bila ya kufungua kifua wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kutembelea JKCI jana kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa. Kulia kwa Dk. Nkya ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Dk. Faustine Ndugulile Mbunge wa Kigamboni .Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi Dk. Faustine Ndugulile Mbunge wa Kigamboni akizungumza na vyombo vya habari wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kutembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jana kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa.Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Alex Joseph akiwaeleza wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi aina za upasuaji wa moyo zinazofanyika katika Taasisi hiyo wakati kamati hiyo ilipotembelea JKCI jana kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa.