NA FREDDY MARO,AICC,ARUSHA
KIKAO kazi cha nne cha Serikali Mtandao (e-GA) kimeanza leo Jumanne Februari 6,2024 katika Ukumbi wa Kimtaifa wa Mikutano wa Simba-AICC,Arusha.
Kikao hicho kimefunguliwa rasmi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.George Simbachawene.
Wakati wa kikao hicho Waziri Simbachawene amesisitiza umuhimu wa Taasisi zote za Umma kufanya kazi zao kwa kutumia Mifumo ya TEHAMA ili kutoa huduma bora na kwa wakati kwa Umma wa Watanzania.
Jumla ya Wajumbe zaidi ya 1300 wanahudhuria Kikao kazi hicho