NA MWANDISHI WETU, DODOMA
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali Dk Eliezer Mbuki Feleshi ametembelea banda la Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, watumishi wa Ofisi ya Kamishna wa Ardhi nchini na Mabaraza ya Ardhi na Nyumba wamepata fursa ya kumueleza huduma wanazotoa kwa wananchi.
Aidha, wananchi wanakaribishwa kwenye banda hilo kupata elimu na huduma kuhusu masuala ya ardhi wakati wa Wiki ya Sheria inayofanyika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma kuanzia Januari 24 – 30, 2024.